TANGAZO TANGAZO TANGAZO TANGAZO
MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA JIJI LA ARUSHA ANAWATANGAZIA WAMILIKI WOTE WA BIASHARA NA MAKAMPUNI YOTE NDANI YA JIJI LA ARUSHA KULIPA KODI NA TOZO MBALIMBALI AMBAZO NI PAMOJA NA USHURU WA HUDUMA (SERVICE LEVY),LESENI ZA BIASHARA,USHURU WA NYUMBA ZA KULALA WAGENI NA USHURU WA LESENI ZA VILEO PAMOJA NA KODI NA TOZO ZOTE ZA HALMASHAURI KWA MUJIBU WA SHERIA KABLA YA TAREHE 18/02/2019 MUDA UKIPITA SHERIA ITAFUATA MKONDO WAKE NA ADHABU ITATOLEWA KWA WATAKAOKAIDI AGIZO HILI.
AIDHA WAPANGAJI WOTE WA STENDI NDOGO,STENDI KUU,RANGER SAFARI,SOKO KUU,KILOMBERO,KIJENGE NA SANAWARI MNAKUMBUSHWA KULIPIA KODI YA PANGO KABLA YA TAREHE 18/02/2019 HATUA KALI ZITACHUKULIWA KWA WATAKAOKAIDI IKIWA NI PAMOJA NA KUFUNGA MADUKA YOTE .
LIPA KWA WAKATI KUEPUKA USUMBUFU.
“TIMIZA WAJIBU WAKO LIPA KODI KWA MAENDELEO YA JIJI LA ARUSHA”
LIMETOLEWA NA:
MKURUGENZI JIJI LA ARUSHA
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa