• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Arusha City Council
Arusha City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Fedha na biashara
      • Utumishi na Utawala
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Afya
      • Mifugo na Uvuvi
      • Primary Education
      • Elimu Sekondari
      • Usafishaji na Mazingira
      • Works and Infrastucture
      • Water
      • Mipango, Uchumi na takwimu
      • Mipango miji
      • Maendeleo na Ustawi wa Jamii
    • Vitengo
      • Sheria
      • Tekinolojia ya habari Mawasiliano na Mahusiano
      • Manunuzi
      • Internal Audit
      • Uchaguzi
      • Ufugaji wa nyuki
    • Kata
      • Baraa
      • Daraja II
      • Elerai
      • Engutoto
      • Kaloleni
      • Kati
      • Kimandolu
      • Lemara
      • Levolosi
      • Moivaro
      • Moshono
      • Murriet
      • Ngarenaro
      • Olasiti
      • Olmoti
      • Oloirien
      • Osunyai
      • Sakina
      • Sekei
      • Sinon
      • Sokon I
      • Sombetini
      • Terrat
      • Themi
      • Unga Ltd
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Usafi wa Mazingira
    • Elimu
    • Biashara
    • Maendeleo ya Jamii
    • Leseni
  • Madiwani
    • Orodha ya Wahe.Wabunge na Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Maadili
      • Kudhibiti UKIMWI
    • Ratiba
      • Ratiba za Vikao
      • Ratiba ya kumuona Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu za Maombi
    • Mkataba wa huduma kwa wateja
    • STUDY ONLINE
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Hotuba
    • Taarifa kwa umma

MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI

Posted on: March 9th, 2020

MKUU  wa Wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro amewaomba wanawake kutowaamini watoto wa kiume wa ndugu zao na kuwaachia watoto wao kulea ili kupunguza idadi ya matukio ya vitendo vya ubakaji na ulawiti  vinavyoshamiri wilayani humo.

Ombi hilo alilitoa  leo  jijini Arusha wakati akizungumza na akina mama wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani, ambayo kitaifa yalifanyika Machi 8 na kwa upande wa Halmashauri ya Jiji la Arusha yameadhimishwa Machi 9 mwaka huu.

Alisema  familia nyingi zinakumbwa na matukio hayo sababu ya kuwaamini kupita kiasi watoto wa mjomba,dada na ndugu wengine, jambo ambalo kwa sasa kila mmoja anapaswa kuacha na kuchukua tahadhari.

"Mimi nawaomba akina mama acheni kabisa kuamini watoto wa ndugu kwani matukio mengi ya ubakaji na ulawiti yanafanywa na watoto wa ndugu, tena ikiwezekana chukueni tahadhari hata kwa baba wa hao watoto wenu maana wengine baadhi wanabaka na kuwalawiti watoto wao wa kuwazaa

yaani msiamini mtu kupita kiasi,"alisema.

Aidha aliwasihi wanawake kusaidiana kurudisha jamii  kwenye maadili kwani yameporomoka kuzidi kiasi.

"Mi hapa napo nawaomba tusaidiane kuwarudisha watoto wetu kwenye kuwajenga kiroho kwa kuwahimiza kwenda nyumba za ibada kanisani au msikitini kutegemea na imani ya kila familia kwa kufanya  hivi itatusaidia sana kujenga taifa lenye hofu ya Mungu na kuwa na maadili mema katika jamii,"alisema.

Pia alikemea jamii za wafugaji pembezoni mwa Jiji kuacha kubagua watoto kwa kusomesha watoto wa kiume pekee na kudharau wakike.

Daqarro alisema ni vema kila mtu akafahamu mtoto wa kike akisoma jamii nzima imeelimika na asilimia kubwa ndio viongozi wazuri wa baadaye na waangalizi wa familia tofauti na watoto wa kiume.

Alisisitiza lazima kila familiya ikazingatia usawa wa kijinsia na kukemea mila na desturi zilizopitwa na wakati.

Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Chama cha Mapimduzi (UWT) Mkoa wa Arusha, Yasmin Bachu aliwaomba wanawake kupendana na kuacha chuki miongoni mwao ili wasaidiane kushika nafasi mbalimbali za uongozi kwenye uchaguzi mkuu mwaka huu.

"Mwaka huu kuna uchaguzi mkuu jitokezeni kugombea nafasi mbalimbali na nawaomba tumpe heshima Rais  John Magufuli katika uchaguzi wa mwaka huu, tusirudie makosa ya mwaka 2015 tuliyofanya,"alisema.



Matangazo

  • Tangazo la zoezi la utoaji wa Vitambulisho kwa njia ya mtandao laanza, wajasiriamali wenye vigezo kusajili. April 06, 2021
  • Tangazo la Nafasi za kazi Halmashauri ya Jiji la Arusha July 17, 2018
  • Wanafuzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza 2019 chaguo la pili Halmashauri ya Jiji la Arusha January 04, 2019
  • Tangazo la Mkutano wa kawaida wa Baraza la Madiwani (Robo ya Pili) Tarehe 30/1/2019 January 25, 2019
  • Tazama zote

Habari za hivi punde

  • MAAFISA MAENDELEO JIJI LA ARUSHA WATAKIWA KUPINGA UKATILI

    March 16, 2021
  • MBUNGE MAGIGE ATOA MIFUKO 100 YA SARUJI UJENZI SEKONDARI UNGALIMITED

    March 14, 2021
  • WATENDAJI KATA NA WATAALAM WA AFYA WATAKIWA KUSAIDIA HUDUMA YA AFYA

    March 12, 2021
  • SERIKALI YARIDHISHWA NA MIRADI YA MIUNDO MBINU JIJINI ARUSHA

    March 10, 2021
  • Tazama zote

Video

ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • MIRADI ILIYOKAMILIKA
  • MKATABA WA HUDUMA KWA WATEJA
  • SISI NI NANI

Viunganishi Linganifu

  • TAMISEMI
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Utumishi
  • Tovuti ya ajira
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Counter

Location Map

Wasiliana nasi

    20 Boma Street 23101

    Sanduku la Posta: 3013

    Simu: 0272548072

    Simu ya Mkononi: 0272545768

    Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa