Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha ni Dkt. John Marco Pima.
Kitaaluma, ni Mtafiti katika fani ya Sayansi ya Teknolojia ya Habari katika Nyanja za “Blended Learning”, Elimu Mtandao; “E-Government”; na “E-Records and Archival Management”.
Dkt. Pima ana uzoefu wa uongozi katika nafasi za uandamizi kwa zaidi ya miaka mitano na amepata mafunzo mbalimbali ya kiuongozi, kimkakati na kijamii.
Kabla ya kuteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha, Dkt. John Pima alikuwa Mkurugenzi mtendaji katika Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua tangu Julai 2016 hadi Juni 2020.
Pia amekuwa Mhadhiri katika Chuo Cha Uhasibu Arusha tangu mwaka 2006.
Dkt. John Pima anayo Shahada ya Uzamili (Masters) ya Sayansi ya Kompyuta toka Chuo Kikuu cha Coventry, Uingereza. Dkt. Pima amehitimu Shahada ya Uzamivu (PhD in Computing) akibobea katika fani ya “Blended Learning” na “Collaborative Web Technologies”. Dkt Pima amewahi pia kuwa Meneja wa TEHAMA (ICT Manager) katika Chuo Cha Uhasibu Arusha tangu mwaka 2012 hadi 2016.
Amefanya tafiti mbalimbali na kuchaptisha maandiko yake katika majarida na makongamano ya kitaifa na kimataifa. Kwa sasa Dkt. Pima amejikita zaidi katika kusimamia maendeleo ya Halmashauri ya Jiji la Arusha.
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa