IDARA YA KILIMO, UMWAGILIAJI NA USHIRIKA
Halmashauri ya Jiji ina ukubwa wa Hekta 20,800 na eneo linalofaa kwa Kilimo ni Hekta 13,520 hata hivyo eneo lililolimwani Hekta 12,265 na wakulima wapatao 112,943. Mahitaji ya chakula kwa Jiji ni Tani 124,932.6 kwa mwaka na uwezo wetu ni wa kuzalisha nafaka ni Tani 21.352 na mazao ya mikunde ni Tani 3,875 wakati matunda na mboga mboga ni Tani 3,468.
Kutokana na hadhi ya Jiji tuliyonayo na pia eneo kubwa kuwa Mji tumejikita zaidi katika kuhamasisha uzalishaji wa mazao ya bustani (mboga mboga na matunda).
Shughuli hizi za Ugani zimeboreshwa zaidi kwa kuanzisha mashamba darasa 18. (16 Ufagaji Kuku na 2 kilimo cha mboga mboga). Pia Idara ya Kilimo inaendelea kuhamasisha usindikaji wa mboga na matunda ili kuongeza thamani ya mazao na vikundi 4 vinaendelea kuimarishwa ili viweze kuzalisha bidhaa zenye ubora na viwango vinavyohitaji katika soko.
PEMBEMBEJEO ZA KILIMO
Zinapatikana kwa wingi kwenye Maduka ya Pembejeo yaliyopo katika Jiji la Arusha. Kuna jumla ya Maduka 112 yanayouza Pembejeo mbalimbali za Kilimo kama Mbolea, Mbegu na Madawa.
Maeneo ambayo Pembejeo zinaweza kupatikana kirahisi na kwa bei nafuu ni pamoja na Kata ya Kati, Sokon I, Levolosi, Kimandolu, Baraa, Moshono na Murriet
ZANA ZA KILIMO
Zana za Kilimo zinazopatikana katika Jiji letu hutumiwa na Wakulima wote wa Jiji hili wapatao 112,943.
Zana hizo ni kama;
MATUMIZI BORA YA MBOLEA
Kila mkulima anapaswa kutumia mbolea ili kuongeza uzalishaji wa mazao. Mbolea inayopaswa kutumiwa ni ile iliyobeba virutubisho tarajiwa. Kila mkulima anapaswa kununua mbolea bora katika maeneo yaliyoainishwa, kutunza na kutumia kwa kufuata maelekezo.
MAMBO YA KUZINGATIA WAKATI WA KUNUNUA MBOLEA
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa