Sunday 22nd, May 2022
@
Maonesho ya biashara yanayojulikana kama sabasaba yalianza mwaka 1962 yakiwa ni maonesho ya Kilimo yaliyokuwa yakifanyika katika viwanja vya Wizara ya Biashara na Ushirika.Maonesho hayo yalikuwa na lengo la kukuza kilimo na ushirika.
Mwaka 1978 serikali iliunda Bodi ya Biashara ya nje kupitia sheria yake namba 5 ya mwaka huo,Bodi hiyo ilipewa mamlaka kushughulikia usafirishaji wa bidhaa za kitanzania nje ya nchi.Bodi ya Biashara ya nje ilipewa pia dhamana ya kukuza ushirikiano wa biashara ya kimataifa kupitia maonesho ya kibiashara,kufanya utafiti kuhusiana na biashara.
Miaka ya hivi karibuni maonesho hayo yamekuwa yakishirikisha nchi takribani 20 kutoka kusini mwa Afrika (SADC) vilevile yamejulikana kama maonesho ya Biashara ya Kimataifa Dar es salaam na viwanja vinajulikana kama viwanja vya Maonesho vya Mwalimu Nyerere.
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa