UTARATIBU WA KUPATA LESENI ZA BIASHARA
Leseni zote za Biashara hutolewa chini ya Sheria ya Biashara Na. 25 ya mwaka 1972 na marekebisho yake yaliyofanyika mwaka 2014 Mwombaji wa Leseni ya biashara anapaswa ajaze fomu ya maombi ya leseni TFN 211 (Business license application form). Moja ya kazi kubwa ya Kitengo hiki ni kurasimisha Biashara zote, kukuza biashara, kuelimisha Umma na kukusanya Tozo mbalimbali za Leseni kuwasaidia wajasiriamali kutambua fursa mbalimbali ikiwemo Masoko kwa bidhaa zoa.
MASHARTI YA KUOMBA NA KUPEWA LESENI ZA BIASHARA
MALIPO
Serikali ilirudisha rasmi utoaji wa ada za Leseni za biashara kupitia Sheria ya Fedha Na. 5 ya mwaka 2011. Kutokana na marekebisho hayo, utaratibu wa kutoa Leseni za biashara bila malipo uliondolewa na kurudishwa ada ya Leseni kuanzia 30 Juni, 2013.
Kiwango cha ada ya Leseni kinatofautiana kulingana na aina ya biashara husika na eneo ilipo biashara hiyo. Mfano : kiwango cha ada za Leseni kwa Halmashauri ya Jiji na Manispaa ni tofauti na za Halmashauri ya Wilaya na maeneo ya Vijijini. Baada ya ulipaji wa ada hiyo mfanyabiashara atapatiwa stakabadhi kwa malipo halali ya Fedha yake.
ADHABU
Mfanyabiashara atakayekutwa anafanya biashara bila kuwa na Leseni atatozwa faini isiyopungua 200,000/= na isiyozidi 1,000,000/= au apelekwe Mahakamani hii imeainishwa kutoka kufungu Na. 10 (1) (b).
WAJIBU WA MFANYABIASHARA
AINA ZA LESENI
Biashara ya Vileo inatekelezwa kufuata Sheria ya mwaka 1968, Kifungu 28 (Liquor License Act No. 28 of 1968) na marekebisho ya Sheria hiyo yaliyofanywa mwaka 2004.
UTARATIBU WA UPATIKANAJI WA LESENI ZA VILEO
Maombi yote mapya ya Leseni za Vileo ni lazima yapitishwe na wataalam ambao wameainishwa kwenye Fomu ya maombi (Afisa Mtendaji, Afisa Afya, Afisa Mipango, Afisa Biashara, Mamlaka ya Leseni.
Maombi yote yanayorudiwa (Renewal) yawasilishwe moja kwa moja kwa Afisa anayeshughulikia Leseni za vileo kwa utekelezaji.
Leseni za Vileo hutolewa kwa vipindi viwili (2) kwa mwaka ambapo kipindi cha kwanza huanzia tarehe 01/04 hadi 30/09 na kipindi cha pili huanzia tarehe 01/10 hadi 31/03 mwaka unaofuata. Leseni za Vileo hutolewa kwa mujibu wa Sheria na huendeshwa kwa muda maalumu kulingana na siku au matukio mfano, sikukuu na siku za mapumziko si sawa na siku za kazi.
MUDA WA KUFANYA BIASHARA ZA VILEO
Jumatatu hadi Ijumaa:
Kuanzia saa 6:00 mchana. (Biashara hupaswa kufungwa), Hufunguliwa tena saa 11: 00 jioni hadi saa 5:00 usiku.
Jumamosi, Jumapili na Sikukuu:
Biashara hufunguliwa saa 06 mchana hadi 08 mchana (Biashara hupaswa kufungwa) Hufunguliwa tena 11 Jioni hadi 6 usiku.
NB: Kutozingatia muda huo au kufanya biashara ya Vileo kwa mazoea na
Kupitisha muda ni kosa linalopaswa kuchukuliwa hatua.
Sheria hii haihusiwi kwa wale wanaomiliki Leseni halali za NIGHT CLUB.
Aidha wanaoendesha biashara ya Vileo bila kufuata taratibu zilizotajwa hapo juu huchukuliwa hatua za Kisheria ikiwa ni pamoja na kupelekwa Mahakamani, kulipishwa faini pamoja na penalty au kufungiwa biashara zao.
Leseni hii hutolewa chini ya Sheria Na. 25 ya mwaka 1972 na marekebisho yake ya mwaka 2014.
MABADILIKO YA MSIMU WA LESENI
Kwa sasa Leseni hutolewa kwa kuzingatia muda wa uanzishwaji wake ili kuishia mwaka unaofuata siku moja kabla. Hii ni faraja kubwa kwa wafanyabiashara wetu ukilinganishwa na mfumo wa awali ambapo kila mwenye Leseni mpya alipaswa kuanzia Julai Mosi na kuishia Juni, 30 mwaka unaofuata wa Fedha.
Hii ni kwa maombi mapya ya Leseni tu, wengine wataendelea na taratibu za awali kama kawaida.
Pia ikumbukwe siku 21 baada ya tarehe ya kwisha msimu wa Leseni yako, utapaswa kulipia adhabu ya 25% na ongezekeko la 2% kila mwezi.
Ukaguzi wa Leseni hufanywa kwa mujibu wa Sheria, na hufanywa wakati wowote inapoonekana inafaa na bila ya kutoa taarifa kwa mfanyabiashara. Adhabu yaweza kuwa faini ya papo kwa papo. Kufungiwa kuendesha biashara, kupelekwa Mahakamani au vyote kwa pamoja.
FAIDA ZA MFANYABIASHARA KUWA NA LESENI NI PAMOJA NA:-
NB: Kwa maelezo zaidi na Ushauri juu ya yote yahusuyo biashara yako usisite
Kufika Ofisi ya Biashara Jiji la Arusha chumba nmba 16 na 18 au kuwasiliana.
Afisa biashara wa Jiji moja kwa moja.
MAFANIKIO YA KITENGO:-
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa