Majukumu ya Idara ni kutoa michango ya kimkakati kwa Menejimentikatika mambo yahusuyo Utawala na Menejimenti ya Rasilimali Watu kama ajira, uendelezaji rasilimaliwatu, uelimishaji, upandishaji vyeo, menejimenti ya utendaji kazi na kushughulikia maslahi ya watumishi.
Idara inatunza na kuhuisha kumbukumbu za rasilimali watu na kutoa huduma za kiutawala ili kuhakikisha mazingira mazuri ya kufanyia kazi.
Kuhakikisha kuwa utumishi wa umma unaendeshwa kwa kuzingatia sera,sheria, kanuni, taratibu na miongozo mbalimbali katika utumishi wa umma;
kufuatilia na kutafsiri sera, sheria, kanuni, taratibu na miongozo yautumishi wa umma na kusimamia uwianishaji wa ajira katika utumishi wa umma ndani ya Halmashauri kwa kufuata kanuni na taratibu zote zilizowekwa na Serikali.