MAJUKUMU YA KITENGO CHA SHERIA
1. Kufuatilia ,Kusimamia na kutetea kesi za Halmashauri ya
Jiji zilizoko Mahakamani baada ya siku 1 tu kuwepo kwa
kesi hizo Mahakamani na kuzingatia taratibu za uendeshaji wa
kesi Mahakamani .
2. Kuandaa na kusajili nyaraka za kimahakama zinazohusiana na
kesi zilizoko Mahakamani baada ya siku 21 baada ya kupokea
hati za madai .
3. Kusimamia sheria mama na sheria ndogo za halmashauri kwa
kuchukua hatua za kisheria kwa wanaokiuka sheria ndani ya
mamlaka ya Halmashauri ikiwa ni pamoja na kuwafikisha polisi
na Mahakamani baada ya kuwapatia notisi ya siku 30 za kutii
sheria zilizopo na kuonekana wanakaidi.
4. Kuandaa rasimu ya sheria Ndogo na au kufanya marekebisho ya
sheria Ndogo zilizopitwa na wakati ndani ya siku 7 baada ya
kupata mapendekezo kutoka kwenye menejimenti.
5. Kutoa elimu au taarifa kwa umma kuhusu sheria Ndogo za
Halmashauri zinazokusudiwa kutungwa siku 14 kabla ya
halmashauri kupitisha sheria hizo.
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa