Katibu Tawala Wilaya ya Arusha Khamana Simba amewataka walimu kuhakikisha vipindi vya michezo vinatumika kufundisha michezo na sivinginevyo.
Ameyasema hayo alipokuwa akizindua mashindano ya UMISSETA na UMITASHUMTA katika Wilaya ya Arusha na maadhimisho ya miaka 50 ya ushiriki katika mashindano hayo.
Amesema kuna baadhi ya Walimu wanageuza vipindi vya michezo kufundishia masomo mengine.
"Inashangaza kuona baadhi ya walimu wanafuta vipindi vya michezo nakufundisha masomo mengine".
Hivyo, amewataka walimu wote kusimamia kwa umakini vipindi vya michezo kwa wanafunzi.
Amesema kwa kufanya hivyo kutasaidia kuibua vipaji vya michezo mbalimbali kwa wanafunzi nakuweza kuwaendeleza.
Amesisitiza kuwa ili timu zote ziweze kushinda katika michezo hiyo nilazima wajipange vizuri na kushirikiana.
Pia, amewataka wanafunzi wawe na nidhani, utii, kusoma kwa bidii, wajitunze, wapende michezo na kujiepusha na vitendo viovu.
Kamala amesema michezo ni afya na inasaidia kuwaepusha wanafunzi kufanya vitendo viovu.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Afisa Elimu Msingi Hussein Bakari amesema Halmashauri ya Jiji itaendelea kutoa ushirikiano kwa wanafunzi na walimu ili kuhakikisha timu zinashiriki kikamilifu kwenye mashindano hayo.
Kwa upande wake, Afisa Utamaduni, Sanaa na Michezo Jiji la Arusha Lucy Jiranga amesema,timu za michezo za Halmashauri ya Jiji la Arusha zimekuwa zikishiri mashindano hayo tokea mwaka 1974 na mwaka huu 2024 zinatimiza miaka 50.
Amesema Ofisi ya Mkurugenzi wa Jiji la Arusha kwa mwaka 2023 ilifanikiwa kununua Mipira ya Miguu na jezi kwa timu zilizoshiriki mashindano ya UMISSETA na UMITASHUMTA 2023.
Katika mashindano hayo timu 7 za Halmashauri ya Jiji ziliweza kushika nafasi mbalimbali kwa mpira wa Mikono wasichana walikuwa washindi 2,mpira wa Pete washindi 2, Mpira wa Kikapu wavulana washindi 3,Mpira wa Kikapu wasichana washindi 3, na fani za ndani washindi wa 1.
Uzinduzi wa mashindano ya UMISSETA na UMITASHUMTA ngazi ya Wilaya yamezinduliwa rasmi ikiwa imejumuisha timu 6 kutoka shule za Sekondari na timu 5 Shule za Msingi katika michezo mbalimbali.
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa