Aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha Bw. Hargeney Chitukuro leo Juni 13,2023 amekabidhi rasmi Ofisi kwa Mkurugenzi mpya wa Halmashauri hiyo, Eng. Juma Hamsini.
Eng. Juma Hamsini amepangiwa kuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha kufuatia uteuzi uliofanywa tarehe 07 Juni , 2023 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Akikabidhi Ofisi hiyo kwa Mkurugenzi mpya, Bw. Chitukuro aliwashukuru Wakuu wa Divisheni/Vitengo wa Halmashauri hiyo kwa muda wote waliofanya kazi pamoja na kumwonesha ushirikiano mkubwa na kuahidi kuendelea kushirikiana nao katika majukumu mengine ya kikazi.
Naye Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Eng. Juma Hamsini aliwasisitiza Wakuu hao wa Divisheni/Vitengo kusimamia miradi kwa weledi na ufanisi na kusema kuwa ni lazima miradi hiyo inayotekelezwa iendane na thamani ya pesa na ubora wa hali ya juu.
Aidha, akizungumza kwa niaba ya wakuu wa Divisheni/Vitengo wa Halmashauri ya Jiji hilo Mkuu wa Idara ya fedha, Joshua Mnyaluko alimshukuru aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi Bw. Hargeney Chitukuro kwa Ushirikiano na kumuomba Mkurugenzi mpya kuwafungulia milango ya kuwasikiliza kwa ushauri na mambo mbalimbali ya kiutendaji.
PICHANI: Katikati ni Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Jiji ya la Arusha Mhe. Maxmillian Matle Iranqhe akiwa na Aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi wa Jiji hilo Bw. Hargeney Chitukuro (wa kwanza kushoto) na Mkurugenzi mpya wa Halmashauri hiyo Eng. Juma Hamsini (wa kwanza kulia) wakati wa makabidhiano ya Ofisi yaliyofanyika mapema leo.
PICHANI : Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, Eng. Juma Hamsini akizungumzia na Wakuu wa Divisheni na Vitengo wa Halmashauri ya Jiji la Arusha wakati wa makabidhiano ya ofisi hiyo.
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa