ARUSHA JIJI WANUFAIKA NA MRADI MPYA, BARABARA, STENDI NA SOKO KUJENGWA
KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, imetoa rai kwa Ofisi ya Rais-TAMISEMI kuhakikisha inasimamia kwa weledi fedha zilizoletwa kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa TACTIC ili uweze kukamilika kwa wakati na kuleta tija kwa wananchi.
Hayo yamesemwa jijini Arusha na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe Denis Londo wakati wa ziara ya kamati hiyo kukagua miradi iliyotekelezwa kupitia TSCP ambayo ni ujenzi wa Dampo (Muriet) pamoja na uwanja wa michezo Ngarenaro na kazi zitakazofanywa kupitia Mradi wa TACTIC ambayo ni Barabara ya Oljoro-Muriet na Barabara ya Bypass Kisongo-Airport, Ujenzi wa Stende eneo la Bondeni Seed na ukarabati wa Soko la Kilombero ambayo inasimamiwa na Ofisi ya Rais-TAMISEMI.
Mhe Londo amesema Jiji la Arusha ni miongoni mwa maeneo yaliyobahatika kupokea fedha za mradi huo na hivyo kusisitiza kuwa ni vema fedha hizo zikatumika kwa weledi ili kutimiza azma ya serikali ya kuwahudumia wananchi wake.
" Arusha imebahatika kupata mradi huu ni matumaini yetu kuwa fedha hizi ambazo Rais wetu Dkt Samia Suluhu Hassan amezitafuta na kuzileta basi zisimamiwe kwa weledi ili ziweze kukamilisha miradi hii kwa wakati na kuleta tija kwa Taifa letu," Amesema Mhe Londo.
Kwa upande wake Naibu Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe Deogratius Ndejembi ameiahidi kamati hiyo kuwa watahakikisha miradi hiyo inasimamiwa kwa weledi na kukamilika katika muda uliopangwa lengo likiwa kutimiza azma ya serikali ya awamu ya sita ya kuwahudumia wananchi wake.
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa