Baraza la Madiwani Halmashauri ya Jiji la Arusha limepitisha Bajeti ya Bilioni 51kutoka katika mapato ya ndani kwa mwaka 2024/2025.
Maamuzi hayo yamefikiwa na Baraza hilo katika kikao cha Bajeti kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari kwa niaba ya Madiwa wote Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha Maximilian Iranqe baada ya baraza hilo amesema iyo ni Bajeti kubwa kuliko bajeti nyingine zilizopita.
Katika Bajeti hiyo, vipaombele vitakuwa katika Sekta ya Elimu, Afya na Miundombinu kwani maeneo hayo ndio yanawagusa wananchi moja kwa moja.
Amesema, Bilioni 1.4 itakwenda katika maendeleo,Bilioni 2 ni fedha zakununua mitambo yakukarabati barabara zilizopo chini ya Halmashauri hiyo.
Pia, Amesema katika Bajeti hiyo Halmashauri imepanga kufunga taa za Barabara katika Jiji lote, kuboresha Masoko,kujenga uwanja mdogo wa mpira wa Miguu na kununua Timu ya Mpira wa Miguu ya Jiji la Arusha.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha Mhandisi Juma Hamsini amesema, jumla ya Bajeti yote ya Halmashauri ni Bilioni 137 ikiwa imejuisha Mapato ya ndani Bilioni 51 na fedha nyigine kutoka kwa Wahisani na Serikali Kuu.
Amesema Halmashauri imejipanga kuongeza makusanya kutoka vyanzo vyake mbalimbali kama vile; kodi za upangishaji wa maduka na Masoko.
Maboresha hayo yatapelekea ongezeko la Mapato ya ndani kutoka Bilioni 48 kwa mwaka wa fedha 2023/2024 hadi Bilioni 51kwa mwaka 2024/2025.
Mkurugenzi amesisitiza zaidi kufanya maboresho kwenye Maeneo mbalimbali ikiwemo Stendi ndogo kwa kujenga jengo la kisasa litakaloweza kupangisha wafanyabiashara takribani 2000 toka 400 waliopo sasa.
Ongezeko hilo litaongeza mapato ya Halmashauri kutoka Bilioni 1.2 kwa sasa hadi Bilioni 6.
Aidha, ameishukuru Kamati ya ulinzi na Usalama ya Wilaya na Mkoa kwa kusimamia makusanyo ya mapato ndani ya wiki moja kiasi cha Milioni 350 zimekusanywa.
Baraza la Madiwani lililopitisha Bajeti hiyo lilishirikisha Waheshimiwa Madiwani, Katibu Tawala wa Wilaya na Wataalamu kutoka Halmashauri ya Jiji la Arusha.
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa