Na Mwandishi Wetu,
Arusha.
Benki ya NMB imetoa msaada wa mabegi 100 kwa wanafunzi wanatoka kwenye familia duni na kuyakabidhi kwa Mkurugenzi wa Jiji la Arusha ikiwa ni muendelezo wa zoezi lililofanywa na ofisi ya Jiji wa kutoa sare pamoja na vitaa vya shule kwa wanafunzi 416 walioshindwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka huu kutokana na kukosa mahitaji hayo.
Akipokea vifaa hivyo leo ofisini kwake, Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Dkt John Pima amesema wanashukuru kuona wadau wa maendeleo wanaona umuhimu wa elimu na kuendelea kutoa sapoti kwa wanafunzi wanaoshindwa kujiunga na shule au kushindwa kuendelea na masomo kutokana hali ngumu ya maisha.
“Msaada huu utaenda kufanya mabadiliko makubwa kwa watoto wetu, lakini licha ya kunikabidhi hii leo, tayari tumeshakaa na Mkuu wetu wetu wa Wilaya na tukaamua kuandaa siku maalum ambayo watoto wenye uhitaji pamoja na waheshimiwa madiwani watakuwepo ambayo ni tarehe 24/02/2022” amesema Mkurugenzi.
Amesema kwenye zoezi la awali la kukabidhi vifaa hivyo lililofanyika katikati mwa mwezi Januari, wanafunzi 416 walipatiwa sare sa shule, madaftari, kalamu, mabegi ya shule pamoja na taulo za kike ambapo hadi kufikia leo hii tayari sare za wanafunzi 413 zimeshakamilika kwa maana ya kushonwa.
Naye Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Kaskazini Dismas Prosper amesema msaada huo umetokana na michango ya wafanyakazi wa benki hiyo ambapo jumla ya shilingi milioni mbili, laki mbili na elfu ishirini zimepatikana na kwamba zoezi la kuchangisha kwa wafanyakazi wengine linaendela.
“Msaada huu tumeutoa kama wazazi, na ndiyo maana tukaamua kuchangishana kama ambavyo tunavyotoa msaada kwa wahitaji mara tatu au nne kila mwaka, hivyo kwa wanafunzi wetu hawa tutaendelea kuwasaidia kadri tutakavyoajaaliwa” Alisema Prosper.
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa