Ni kauli mbiu ya mwaka huu katika kuadhimisha siku ya UKIMWI duniani ambayo kufanyika Tar. 1 Mwezi wa 12 kila mwaka ambapo Halmashauri ya jiji la Arusha imeadhimisha siku hii kwa kufanya maandamano yaliyobeba jumbe mbalimbali zinazohusiana na masuala ya UKIMWI pamoja na kuratibu shughuli za upimaji afya bure na uchangiaji wa damu salama katika viwanja vya Shule ya Msingi Ngarenaro iliyopo jijini hapa.
Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mh. Gabriel Daqarro ndiye mgeni rasmi katika madhimisho hayo ambapo katika hotuba yake alisisitiza jamii kutowanyanyapaa watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi pia kila mmoja anatakiwa kujenga utaratibu wa kupima afya yake na endapo atagundulika kuwa na maambukizi ya ukimwi aweze kuchukua hatua za haraka kwa kuwahi dawa ili aimarishe afya yake kwa mustakabali wa jamii inayomzunguka na taifa kwa ujumla.
Mambo mbalimbali yamefanyika katika Tukio hilo la kihistoria ikiwa ni pamoja na zoezi la uchangiaji wa mfuko wa udhamini kama kauli mbiu inavyoeleza kwa ajili ya kusaidia huduma na mahitaji muhimu ya kundi la watu wanaoishi na virusi vya ukimwi (WAVIU).
Vilevile kulikuwa na burudani ya mpira wa miguu uliobeba
ujumbe mahsusi kuhusiana na maadhimisho haya.
kwa mujibu wa tovuti ya takwimu duniani inaonyesha kuwa Leo Dunia inaadhimisha siku ya UKIMWI huku kukiwa na Zaidi ya watu 39,530,090 wanaoishi na Virusi vya UKIMWI na watu zaidi ya 1,540,834 wamefariki kwa Virusi vya UKIMWI.
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa