Mkuu wa wilaya ya Arusha Mhe. Gabriel Daqarro amemwagiza mhandisi Christopher Ngowi kutoka kampuni ya Ravji Construction Ltd kuwa ifikapo tarehe 14/08/2019 ujenzi wa barabara za Serengeti, Leyora na Machame zenye thamani ya shilingi 768,883,500 zinazosimamiwa na wakala wa barabara za mijini na vijijini (TARURA) jijini Arusha ziwe zimekamilika ili zianze kutumika.
Pichani: Barabara ya Meidimu - Nadosoito baada ya kukamilika kwa matengenezo ya sehemu korofi
**********************************************************
Ametoa agizo hilo wakati wa ziara yake aliyoifanya mapema leo hii kukagua maendeleo ya ujenzi wa barabara hizo ulioanza tarehe 14/01/2019.
Dc Daqarro amesema kuwa kasi ya ukamilishaji wa ujenzi wa barabara hizo hairidishi kwani mpaka sasa mkandarasi hajafikisha asilimia hamsini ya ujenzi wa barabara hizo licha ya kuwa amebakiza wiki nne tu kati ya muda wa miezi nane aliyopewa kukamilisha barabara hizo.
Pichani: Maendeleo ya ujenzi wa barabara ya Sanawari inayotarajiwa kukamilika kwa kiwango cha lami
*******************************************
“Ifikapo tarehe 14/08/2019 tunataka tuone lami inateleza ili wananchi wetu waweze kufurahia ahadi wanazopewa na serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli, kushindwa kufanya hivyo tutakuwajibisha” alisema Dc Daqarro
Katika ziara hiyo pia Dc Daqarro alipata fursa ya kutembelea na kukagua ujenzi wa barabara ya Sanawari, daraja (box culvet) katika mto kwenye barabara ya Oljoro- Murriet, matengenezo ya sehemu korofi na ujenzi wa kalvati kwenye barabara za Meidimu, Murriet – Nadosoito na Lolovono pamoja na barabara ya Sojema-Amani.
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa