"Hakuna mtu aliye juu ya Sheria, na kama haki niya mtu tutaipigania usiku na mchana ili mtu apate haki yake".
Kauli hiyo, imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe.Felician Mtahengerwa alipokuwa akifungua Kliniki ya malalamiko ya wananchi katika Wilaya hiyo.
Amesema, Wilaya ya Arusha imetekeleza maagizo ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha Paulo Makonda ya kila Wilaya kusikiliza na kutatua changamoto za wananchi wake na Wilaya ya Arusha imeanza kutekeleza maagizo hayo.
Mtahengerwa amesema, katika kliniki hiyo ya kusikiliza changamoto za wananchi Wilaya ya Arusha imeshirikisha chama cha wanasheria Mkoa wa Arusha ili kuhakikisha kero zote za wananchi zinatatuliwa.
Wilaya ya Arusha imetekeleza maelekezo yalitolewa na Mkuu wa Mkoa kwa kusikiliza kero za wananchi kwa siku 3.
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa