Na Mwandishi Wetu
Arusha
Wazazi na walezi wametakiwa kuacha mara moja tabia ya kuwaachia watoto wao kuangalia maudhui na katuni zisizo na maadili badala yake waongee nao ili kubaini changamoto wanazokumbana nazo mashuleni, majumbani na mitaani ili kudhibiti matukio ya ukatili yanayoibuka kwa kasi hivi sasa.
Wanawake wakifuatilia kwa umakini sherehe za maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, Tarehe 08, Machi 2023.
Akizungumza na wanawake wa Jiji la Arusha katika maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, yenye kauli mbiu ya Ubunifu na Mabadiliko ya Teknolojia,Chachu katika kuleta usawa wa Kijinsia" ambapo Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe. Felician Mtahengerwa alisisitiza endapo mzazi utabaini katika chaneli zinazoonyeshwa zinaviashiria vya ushoga au udhalilishaji wachukue hatua ili kudhibiti matukio ya ukatili.
Alisisitiza wazazi na walezi kutokaa kwenye mitandao ya kijamii na kuwa bize nakazi huku wakiacha watoto wakifanyiwa ukatili watu mbalimbali ikiwemo wadada wa kazi.
"Angalieni katuni mnazowaruhusu waangalie nyingine hazina maadili pia wazazi mnaopeana sukari na kondoo ili kumaliza kesi za ulawiti na ukatili kwa wanawake na watoto nje ya mahakama mikibainika mnafanya misamaha ya ovyo ovyo mtakamatwa"
Wanawake wakifuatilia kwa umakini sherehe za maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, Tarehe 08, Machi 2023.
Vitendo vya ukatikili wa jinsia bado zinaendelea haswa kwa wanawake na watoto ikiwemo watoto wa kiume ambao bado wanasahaulika ingawa nao wanafanyiwa ukatili wa aina mbalimbali.
Takwimu zinaonesha kwa mwaka 2022 vitendo vya ukatili wa kijinsia vilivyoripotiwa 8,647, ukatili wa kisaikolojia 12,515 huku ukatili wa kingono 5,781.
Naye Ofisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Arusha Bi. Blandina Nkini aliishukuru Serikali kwa kutoa mikopo ya Shilingi Bilioni 1,390,193,600 kwa mwaka wa fedha 2022/23 ambapo vikundi vya Wanawake 121,vijana 42 na watu wenye ulemavu 20 wamenufaika.
Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Bw. Hargeney Chitukuro akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe. Felician Mtahengerwa alipowasili katika maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani.
Naye Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Bw. Hargeney Chitukuro aliishukuru Serikali kwa kuendelea kutoa kipaumbele kwa makundi ya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu na kuihakikishia Serikali kuwa wao kama Halmashauri ya Jiji la wataendelea kusimamia na kuhakikisha makundi lengwa yananufaika na kupatiwa mikopo hiyo kwa wakati ili kuwaletea maendeleo.
MATUKIO KATIKA PICHA : Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yalivyopambwa na Wanawake wenye shughuli yao
ARUSHA JIJI, KAZI INAENDELEA!
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa