Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mheshimiwa Said Mtanda amewataka walimu wakuu kusimamia ipasavyo fedha zilizo tolewa kiasi cha Shilingi Bilioni 2 kwaajili ya ujenzi wa madarasa 100 ili kukamilisha ujenzi kwa wakati huku akiwaonya vikali wale ambao wataleta ubadhilifu katika pesa hizo.
Akizungumza na wakuu wa shule za sekondari zipatazo 20 ambazo ndizo zinazo nufaika na fedha hizo Jijini Arusha katika kumbi wa Ofisi yake hii leo, Mhe. Mtanda amewata wakuu hao kuepuka ufujaji wa fedha za uma na kuzielekeza katika miradi kwa wakati muafaka ili kukamilisha miradi kwa wakati ulio kusudiwa.
“Mara nyingi fedha zinapoingia katia akaonti zetu kunakua na ucheleweshaji, kuelekea mahali zinapotakiwa kwenda kufanya kazi, wapo baadhi ya wakuu wa shule, wakuu wa idara ambao unaweza kupita mwezi mzima fedha zipo kwenye akaonti hazijaanza kazi nimewaita niwaambie siku 75 zikifika kila mkuu wa shule akabidhi vyumba vya madarasa” anasema Mtanda.
Aidhaa Mhe. Mtanda ameweka bayana mkakati wao wa kununua malighafi za ujenzi kiwandani kwa shule zote ili kupunguza gharama kubwa za ununuzi wa malighafi, kuokoa fedha za uma kusaidia miradi kikamilika kwa wakati.
“Tunaweza tukaongea nakiwanda cha nondo, tukaongea na kiwanda cha bati, na wazakishaji wengine halafu wakuu hawa wakataja idadi ya nondo au bati ngapi zinazo hitajika tukalipa hapo kiwandani tukapata kwa bei nafuu badala kila shule kununua kivyake na kwa bei tofauti na kuchelewesha kukamilika kwa miradi”
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Jiji la Arusha Ndg. Hargeney Chitukuro ametuma salamu za shukurani na pongezi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa kiasi cha Bilioni mbili (2 bn) kwa Jiji la Arusha kwa ajili ya ujenzi wa vyumba 100 vya madarasa na kwamba wanafunzi wote watao faulu na kujiunga na kidato cha kwanza 2023 wanapata mahali pa kujifunzia.
“Tumekusanyuka hapa na wakuu wa shule kwaajili ya kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa kiasi cha Bilioni kwa Jiji la Arusha kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa tayari tumesha zipokea fedha hizo na tumesha ziingiza kwenye akaoni za shule kwaajili kuanza kufanya kazi lengwa”
Hata hivyo Kaimu Mkurugenzi Jiji la Arusha ameeleza kua ameteua mlezi mmoja kwa kila shule miongoni mwa wakuu wake wa idara ili kurahisisha usimamilizi nay eye mwenyewe kujitwika jukumu la kuzizungukia shule hizo ili kuangalia utendaji wa kamati zilizo teuliwa kwaajili ya kutekeleza miradi hiyo.
Ndg. Maneno Maziku ambaye ni Mchumi Jiji la Arusha anaeleza kua wapo tayari kutekeleza maelekezo ya force account kama ilivyo elekezwa na serikali na kuahidi kwamba kwa wakati huu watafanya vizuri zaidi katika ukamilishaji wa miradi hiyo kuliko walivyo wahi kufanya nyakazi zilizo pita.
Shule zitakazo nufaika na vyumba hivi vya madarasa ni pamoja na shule ya Arusha Day, Arusha Sec, Arusha Terrat, Kimaseki Sec, Elerai, Felix Mrema, Kaloleni, Lemara, Mkonoo, Moivaro, Mrisho Gambo, Muriet Sekondari, Naura, Ngarenaro, Olasiti, Olmoti, Oloirien, Sinoni, Sombetini na Unga l.t.d Huku wastani wa kila darasa ukiwa ni milioni 20.
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa