Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha Dr. Maulid Suleiman Madeni amezindua operesheni maalum ya ukusanyaji wa mapato ya Jiji la Arusha ikiwa ni kuunga mkono jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kuhakikisha kila mfanyabiashara analipa kodi ili kusaidia watanzania wanyonge hususani katika sekta nyeti ya afya na elimu.
Katika operesheni hiyo ya mapato aliyoizindua hapo jana katika Soko Kuu lililopo Jiji la Arusha, Dr. Madeni aliambatana na wataalam mbalimbali wa Halmashauri akiwemo Mweka Hazina wa Jiji Bw. Mwana Msangi, Mchumi wa Jiji Bi. Anna Mwambene, Afisa Biashara Wa Jiji Bw. Godfrey Edward na Mhasibu Wa Mapato Bw. Ben Massangano katika kuhakikisha zoezi linafanikiwa kwa asilimia zote.
Pia Mkurugenzi amempangia majukumu mengine msimamizi wa soko hilo Bw. John Ruzga kwa kushindwa kusimamia mapato ya Halmashauri kwa kukusanya shilingi milioni 23 kwa mwezi badala ya shilingi milioni 31,610 iliyotarajiwa sambamba na changamoto nyingine za wamiliki wa vibanda na vizimba kukodisha wafanyabiashara wengine kinyume na utaratibu.
Operesheni hiyo ni endelevu ambapo Dr. Madeni atafanya ziara katika masoko na vyanzo vyote vya mapato vilivyo chini ya Halmashauri kwa lengo la kuhakikisha wafanyabiashara wote na wamiliki wa vibanda wana leseni za muda husika, risiti halali za kodi na mikataba halali ya halmashauri sambamba na kufungia vibanda kwa wafanyabiashara wote ambao hawana vielelezo vya kutosha.
Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, Dkt. Maulid Madeni (kulia) akiongozana na Afisa Biashara wa Halmashauri ya Jiji wakati wa ziara yake ya kukagua vyanzo mbalimbali vya mapato katika Soko Kuu la Jiji wakati wa ziara yake aliyoifanya jana (Jumatatu Septemba 10, 2018).
Mkurugenzi wa Jiji la Arusha (kulia) akizungumza na mmoja wa Wafanyabiashara wa matunda katika Soko Kuu la Arusha wakati wa ziara yake ya kukagua vyanzo mbalimbali vya mapato katika Soko hilo hapo jana (Jumatatu Septemba 10, 2018) ambapo aliambatana na timu ya watendaji wa Halmashauri ya Jiji hilo.
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa