Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Idd Hassan Kimanta amesema eneo la wazi la Bondeni litatumika kama eneo la mapumziko kwaajili ya wananchi wote wa Arusha.
Ameyasema hayo alipokuwa akikagua eneo hilo lilipo karibu na Msikiti wa Bondeni Jijini Arusha na kuzungumza na wananchi waliokuwepo katika eneo hilo.
“Eneo hili litatumika kwaajili ya wananchi kupumzika na haya ni maelekezo yaliyotolewa na Mhe. Rais John Pombe Magufuli siku aliyotuapisha”.
Aidha,Kimanta amewata waegesha magari wote katika eneo hilo kuondoa magari yao ifikapo Julai Mosi, 2020 ili kuliacha eneo hilo wazi ili Halmashauri ya Jiji la Arusha iweze kulifanyia maandalizi kwaajili ya wananchi kupumzika baada ya shughuli zao za kila siku kwani eneo hilo linamilikiwa na Serikali na nikwaajili ya matumizi ya Umma.
Pia, amewataka wamiliki wa magari yote yaliyokuwa yameegeshwa katika eneo hilo la wazi kutumia eneo la Msikiti wa bondeni kuegesha magari yao kwa kufuata taratibu za eneo la Msikiti.
Mhe. Kimanta pia katika ziara yake amekagua baadhi ya maeneo ya miradi ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa shule ya sekondari ya Arusha Terrati.
Mwisho.
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa