• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Arusha City Council
Arusha City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Fedha na biashara
      • Utumishi na Utawala
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Afya
      • Mifugo na Uvuvi
      • Primary Education
      • Elimu Sekondari
      • Usafishaji na Mazingira
      • Works and Infrastucture
      • Water
      • Mipango, Uchumi na takwimu
      • Mipango miji
      • Maendeleo na Ustawi wa Jamii
    • Vitengo
      • Sheria
      • Tekinolojia ya habari Mawasiliano na Mahusiano
      • Manunuzi
      • Internal Audit
      • Uchaguzi
      • Ufugaji wa nyuki
    • Kata
      • Baraa
      • Daraja II
      • Elerai
      • Engutoto
      • Kaloleni
      • Kati
      • Kimandolu
      • Lemara
      • Levolosi
      • Moivaro
      • Moshono
      • Murriet
      • Ngarenaro
      • Olasiti
      • Olmoti
      • Oloirien
      • Osunyai
      • Sakina
      • Sekei
      • Sinon
      • Sokon I
      • Sombetini
      • Terrat
      • Themi
      • Unga Ltd
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Usafi wa Mazingira
    • Elimu
    • Biashara
    • Maendeleo ya Jamii
    • Leseni
  • Madiwani
    • Orodha ya Wahe.Wabunge na Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Maadili
      • Kudhibiti UKIMWI
    • Ratiba
      • Ratiba za Vikao
      • Ratiba ya kumuona Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu za Maombi
    • Mkataba wa huduma kwa wateja
    • STUDY ONLINE
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Hotuba
    • Taarifa kwa umma

FAHAMU KUHUSU SENSA YA WATU NA MAKAZI 2022

Posted on: May 24th, 2022

FAHAMU KUHUSU SENSA YA WATU NA MAKAZI 2022

SENSA YA WATU NA MAKAZI 2022

Tanzania itafanya Sensa ya watu na makazi 23 Agosti mwaka 2022 siku iliyotangazwa na Mh. Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania. Kabla ya zoezi la kuhesabu watu wote watakaolala ndani ya mipaka ya nchi usiku wa kuamkia siku ya Sensa, shughuli mbalimbali za maandalizi hufanyika ambazo hujumuisha utoaji Elimu kwa lengo la kuelimisha umma juu ya umuhimu wa Sensa ili kuhakikisha kila mmoja anatambua umuhimu wa kuhesabiwa na kuhamasika kuhakikisha kwamba anahesabiwa na anahesabiwa mara moja tu.

Elimu hii inajumuisha mada mbalimbali zikiwemo; Sensa ni nini, Nani anapaswa kuhesabiwa, ni taarifa gani zitakusanywa wakati wa Sensa na umuhimu wa kuweka kumbukumbuku za watu wote waliolala katika kaya usiku wa kuamkia siku ya Sensa. Mambo muhimu unayopaswa kuyafahamu kuhusu Sensa ya Watu na Makazi ni yafuatayo:

  • SENSA YA WATU NA MAKAZI NI NINI?

Sensa ya watu na makazi ni moja ya zoezi linalokusanya taarifa za kila mtu aliyelala ndani ya mipaka ya nchi usiku wa kuamkia siku ya Sensa. Sensa ya Mwaka 2022 kama zilivyo Sensa zilizopita,itahusisha Makarani wa Sensa ambao watatembelea kaya zote nchini na kufanya Mahojiano ya ana kwa ana baina ya Karani wa Sensa na Mkuu wa kaya. Ikiwa Mkuu wa kaya hatakuwepo, karani wa Sensa atafanya Mahojiano na mtu mzima yeyote katika kaya ambae ana taarifa za kutosha kuhusu kaya na wanakaya wenzake waliolala katika kaya husika usiku wa kuamkia siku ya Sensa.

  • NINI LENGO LA SENSA YA WATU NA MAKAZI?

Lengo la Sensa ya watu na makazi ni kupata taarifa sahihi za Kidemografia, Kijamii, Kiuchumi na hali mazingira kwa lengo la kupata takwimu sahihi zitakazoiwezesha serikali na wadau wengine kupanga kwa usahihi mipango ya maendeleo ya watu wake katika sekta mbalimbali za Elimu, Afya, hali ya Ajira ,miundombinu kama barabara, Nishati  na maji safi. Kwa msingi huo, Sensa ni zoezi muhimu ambalo kila mmoja kwa nafasi yake anapaswa kushiriki na kutimiza wajibu wake ili kuhakikisha inakuwa ya mafanikio makubwa. Hii itasaidia serikali kutimiza wajibu wake kwa wananchi kulingana na idadi ya watu ya eneo husika ikiwa kama msingi mkubwa wa ugawaji ya keki ya Taifa kwa kila eneo la utawala hapa nchini.

  • NANI ANAPASWA KUHESABIWA?

Sensa yam waka 2022 kama zilivyo Sensa zilizopita, itafanyika nchi nzima na itahusisha watu wote watakaolala ndani ya mipalaka ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania. Hii inamaanisha kuwa, watu wote watakaolala katika kaya binafsi usiku wa kuamkia siku ya Sensa pamoja na watu wote watakaokuwa katika kaya za jumuiya kama vile hotelini , nyumba za kulala wageni, hospitalini, magereza, mabweni ya wanafuni, kambi za jeshi, vituo vya kuleelea watu wenye mahitaji maalum kama yatima, wazee, kambi za wavivu, watu wasio na makazi maalum,na vituo vya usafiri wa umma (kama vituo vya mabasi, garimoshi, viwanja vya ndege na bandari) watahesabiwa kwa kutumia utaratibu maalum utakaondaliwa na kamati ya Sensa katika ngazi ya mtaa, kitongoji na shehia.

  • NATAKIWA KUFANYA NINI WAKATI WA SENSA YA ATU NA MAKAZI YA MWAKA 2022?

Unachotakiwa kufanya ni kumpa ushirikiano wa kutosha karani wa Sensa atakapokutembelea katika kaya kwa kujibu maswali yote atakayouliza kwa usahihi. Aidha,ukiulizwa swali na hujalielewa au hujasikia vizuri,unayo haki ya kumwomba karani arudie kuuliza au kutoa ufafanuzi ili uweze kutoa jibu sahihi kulingana na swali lililoulizwa. Ni muhimu kwa Mkuu wa kaya kuhakikisha anachukua taarifa muhimu (kama umri, elimu, jinsi, hali ya ndoa, umiliki wa vitambulisho wa Taifa, shughuli za kiuchumi) za watu wote waliolala katika kaya yake usiku wa kuamkia siku ya Sensa ili aweze kukumbuka wakati karani atakapokutembelea katika kaya.

  • SENSA YA WATU NA MAKAZI YA MWAKA 2022 ITAFANYIKA VIPI?

Siku ya Sensa, Karani wa Sensa akiongozana na Mwenyekiti au kiongozi wa Serikali ya Mtaa au Kitongoji/Shehia atafika katika kaya akiwa na kitambulisho cha Karani wa Sensa na Dododso la Sensa lililowekwa katika kifaa cha kielektroniki kiitwacho kishikwambi (Tablet) na kuuliza maswali ambayo yatajibiwa na Mkuu wa kaya. Ikiwa mkuu wa kaya hayupo, mtu mwingine yeyote mzima katika kaya ambaye ana taarifa za kutosha kuhusiana na kaya na watu wote waliolala ndani ya kaya husika usiku wa kuamkia siku ya Sensa anaweza kujibu maswali ya Sensa kwa niaba yake.

  • JE NI TAARIFA ZA AINA GANI ZITAKAZOKUSANYWA WAKATI WA SENSA YA WATU NA MAKAZI YA MWAKA 2022?

Taaridfa zitakazokusanywa zitahusu:

  • Taarifa za kidemografia ( umri,jinsi,hali ya ndoa)
  • Taarifa za ulemavu (aina za ulemavu ,na chanzo cha ulemavu,)
  • Taarifa za uhamaji
  • Taarifa za vitambulisho vya utaifa uhai wa wazazi
  • Taarifa za elimu
  • Taarifa za shughuli za kiuchumi
  • Taarifa za umiliki wa ardhi na TEHAMA
  • Taarifa ya hali za uzazi
  • Taarifa za vifo na vifo vitokanavyo na uzazi
  • Taarifa za nyumba, hali ya umiliki wa nyumba, vifaa/rasilimali na udhibiti wa mazingira
  • Taarifa za kilimo,mifugo,uvuvi na misitu
  • Taarifa kuhusu mpango wa TASAF
  • Taarifa za majengo/nyumba
  • Anwani za makazi
  • Taarifa za huduma za jamii katika ngazi ya kitongoji/shehia na Mitaa.
  • JE, TAARIFA NITAKAZOTOA ZITAKUWA SIRI?

Ndio, kama ambavyo hufanyika katika Sensa na tafiti nyingine za kitakwimu, kwa mujibu wa Sheria ya Takwimu sura 351, taarifa utakazotoa kwa karani wa Sensa zitakuwa SIRI na zitatumika kwa madhumuni ya kitakwimu pekee. Kwa mujibu wa sheria hii, kila karani wa Sensa atasaini kiapo cha kutunza siri za taarifa zote atakazokusanya na chini ya kiapo hicho hatakiwi kutoa taarifa alizotumwa kukusanya kwa mtu yeyote Zaidi ya kuziwasilisha kama zilivyo katika Ofisi ya Takwimu na Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali, Zanzibar. Karani yeyote akithibitika kwenda kinyume na kiapo cha kutunza siri, atashitakiwa na kuadhibiwa kwa mujibu wa sheria hii.

  • NITAMTAMBUAJE KARANI WA SENSA YA WATU NA MAKAZI YA MWAKA 2022?

Karani wa Sensa atafika katika kaya akiwa na kitambulisho na sare maalum inayomtambulisha. Pia ataongozana na Mwenyekiti au kiongozi wa serikali ya Mtaa/kitongoji/shehia.

  • JE, NI WAJIBU KISHERIA KUJIBU MASWALI YA SENSA?

Ndio, kujibu maswali ya Sensa ni matakwa ya Kisheria kwa mujibu wa sharia ya Takwimu sura namba 351.

Kumbuka: Ushirikiano wako wa karani wa Sensa na Watu na Makazi ya Mwaka 2022 kwa kutoa taarifa sahihi ndio utakaorahisisha na kufanikisha Sensa ambapo matokeo yake yatachochea kasi ya maendeleo ya watu na makazi yao katika maeneo yote ya utawala nchini.

  • JE, UVIKO-19 SIYO KIKWAZO CHA KUSHIRIKI KATIKA SENSA YA WATU NA MAKAZI YA MWAKA 2022?

Hapana, UVIKO-19 siyo kikwazo kwa yeyote kushiriki kwa nafasi yake katika Sensa ya mwaka 2022 kwani kulingana na maendeleo ya ugonjwa huu, makarani na watendaji wote katika Sensa hii watazingatia tahadhari zote zinazoelekezwa na Wataalamu wa Afya ili kutokuwaambukiza wananchi au wao kuambukizwa na wananchi wakati wa zoezi la Sensa.

 

Shiriki kikamilifu sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 kwa maendeleo endelevu ya Tanzania

 

SENSA KWA MAENDELEO,

 JIANDAE KUHESABIWA

Matangazo

  • NAMNA YA KUPATA KIBALI CHA KUSAFIRI NJE YA NCHI KWA WATUMISHI WA SERIKALI January 16, 2025
  • MATOKEO YA USAILI WA MCHUJO KADA YA MTENDAJI WA MTAA NA KADA YA MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU October 06, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI October 15, 2024
  • TANGAZO LA MIKOPO October 29, 2024
  • Tazama zote

Habari za hivi punde

  • JIJI LA ARUSHA LAZINDUA MITAMBO MIPYA

    January 28, 2025
  • MKURUGENZI KAYOMBO AKABIDHIWA OFISI

    August 21, 2024
  • WANAWAKE NA WASICHANA KUJENGEWA UWEZO WA KISHIRIKI NAFASI ZA UONGOZI

    August 20, 2024
  • NENDENI MKAONGEZE UFANISI

    August 19, 2024
  • Tazama zote

Video

JIUNGE NA MFUMO WA TAUSI
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • MIRADI ILIYOKAMILIKA
  • MKATABA WA HUDUMA KWA WATEJA
  • SISI NI NANI
  • Urban Sanitation and Hygiene | Mazingira safi Maisha bora

Viunganishi Linganifu

  • TAMISEMI
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Utumishi
  • Tovuti ya ajira
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Counter

Location Map

Wasiliana nasi

    20 Boma Street 23101

    Sanduku la Posta: 3013

    Simu: 0272548072

    Simu ya Mkononi: 0272545768

    Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa