Mwenyekiti wa Kamati ya Uchumi,Elimu na Afya Mhe.Isaya Doitta ambae pia ni Diwani wa Kata ya Ngarenaro amewataka viongozi wa Kata ya Murieti kuhakikisha Watoto wote wanaandikishwa shule badala ya kuzulula mtaani wakati wa masomo.
Kauli hiyo, ameitoa wakati kamati ya Uchumi, Elimu na Afya ya Halmashauri ya jiji la Arusha ilipokuwa ikikagua miradi ya maendeleo.
Amesema Kata ya Murieti inawatoto wengi wanaozulula mitaani wakati wa masomo hivyo inaonesha kuwa Watoto wengi hawajaandikishwa mashuleni.
" Hakuna kitu kinachoniudhi kama kuona Watoto wanazulula tu mitaani badala yakwenda shule", alisema.
Kwa upande mwingine amewataka Walimu na maafisa Elimu kushirikiana kufuta daraja la nne na ziro kwa kidato cha nne na sita.
Amesema kwa kufuta daraja hizo kutaongeza ufaulu wa wanafunzi kwa kiwango kikubwa katika Jiji la Arusha.
Nae, Diwani wa Kata ya Murieti Mhe. Francis Mbise ameishukuru Serikali ya awamu wa sita kwa kuleta fedha nyingi za miradi katika Kata hiyo na pia amempongeza Mkandarasi Laki Contraction Company Limited kwa kufanya kazi nzuri kwenye miradi ya Kata hiyo.
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa