Hali halisi ya uchumi katika familia nyingi kumesababisha jamii kuwa na mabadiliko ya malezi kwa watoto.
Kutokana na mabadiliko ya malezi kwa watoto, kumepelekea ongezeko la matukio ya unyanyasaji wa watoto katika jamii zetu.
Kwani Wazazi wengi wamekuwa na muda mwingi wakutafuta mahitaji ya familia kuliko muda wakukaa na kuwalea Watoto na hiyo kupelekea watoto hao kukosa malezi yenye maadili katika makuzi yao.
Shirika la SOS children's Villange Arusha likishirikiana na Halmashauri ya Jiji la Arusha wamefanya kikao maalumu,kilichowashirikisha Madiwani wa Jiji la Arusha na Viongozi wa dini.
Lengo kubwa, la Kikao hicho ilikuwa kujadili na kupanga mikakati ya pamoja itakayoweza kumkomboa mtoto kutoka katika mazingira hayo ya unyanyasaji kwa kuweka ulinzi wa mtoto.
Bi. Husna Solomi ni Mratibu wa malezi mbadala na ulinzi na usalama wa mtoto kutoka shirika la SOS Children's Village Arusha, amesema, ulinzi wa mtoto umepungua kwa kiasi kikubwa kutoka na mambo mbalimbali ikiwemo utandawazi na mwingiliano wa jamii tofautitofauti.
Pia, kubadilika kwa utamaduni za jamii zetu na elimu, kumepelekea ulinzi wa mtoto kupungua na kuibua vitendo vya unyanyasaji.
Amesema, kutokana na kikao hicho mipango mbalimbali imewekwa ya namna Serikali, Viongozi wa dini na Shirika hilo kwa pamoja watakavyoweza kuwafika watoto katika jamii zao kwa kuwapa elimu.
Bi.Husna amesema, kuwepo kwa nguvu ya makundi hayo matatu kila kundi limeweka mipango ya namna yakuifikia jamii kwa kutoka elimu na kuwasaidia watoto ambao tayari watakuwa wameathirika ili waweze kurudi katika hali ya kawaida.
Mkakati mwingine ambao kikao hicho umeweka ni namna yakuzifikia zile familia zenye watoto walemavu na walezi wao kwa kawapatiwa elimu na kuwakomboka na hali duni ya uchumi, kukandamiza hali na maslahi ya watoto.
Akizungumza kwa niaba ya Madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Arusha, Naibu Meya Abraham Mollel amesema, Baraza la Madiwani litahakikisha idara ya Maendeleo ya Jamii inatengewa bajeti itakayowawezesha maafisa maendeleo ya jamii kutoa elimu katika ngazi za chini.
Amesema, jukumu la kuimarisha ulinzi wa mtoto nila kila mtu hivyo wao kama Madiwani wataendelea kutoa elimu katika kata zao na kupinga vikali unyanyasaji wa watoto.
Amesisitiza kuwa jamii ikiweza kumlinda mtoto itakuwa imeilinda nchi na kutengeneza kizazi chenye kujitambua na kuwajibika na hivyo kuleta maendeleo kwa familia na jamii kwa ujumla.
Kupitia Sheria ya mtoto ya mwaka 2009 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imebainisha namna mtoto anatakiwa kulindwa ili asipoteze haki zake za msingi, na hii ni juhudi ya Serikali katika kuhakikisha mtoto anakuwa salama.
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa