Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe. Gabriel Daqarro akiambatana na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha Dkt. Maulid Madeni leo Tarehe 26 Februari 2020 amefungua Mafunzo ya utoaji mikopo yatakayo tolewa kwa muda wa siku mbili kuanzia Tarehe 26-27 Februari 2020 pamoja na kukabidhi hundi ya mfano ya shilingi 805,686,000 kwaajili ya mikopo itakayotolewa kwa Vikundi 147 vya Wajasiriamali, Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu kwa awamu ya pili ya mwaka wa fedha 2019/2020.
Akiwa mgeni wa heshima katika mafunzo hayo Mhe. Gabriel Daqarro aliviasa vikundi hivyo kuwa mabalozi wazuri watakao hamasisha muitikio mkubwa wa wananchi kujitokeza kuunda vikundi na kujiandikisha ili kupatiwa mikopo, pia alishukuru ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha kwa uandaaji na utoaji wa mikopo hiyo kwani wametimiza maelekezo yaliyoagizwa na Mhe. Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli. Mhe. Daqarro pia aliendelea kusisitiza vijana kujitokeza kwa wingi pale wanaposikia fursa za utoaji mikopo nakuwasihi watumie mikopo hiyo kwa malengo sahihi ili kujiepusha kushinda vijiweni kwani huo ndio mwanzo wa utumiaji wa mihadarati kama madawa ya kulevya. Pia alishauri wana vikundi wote watakao pokea mikopo hiyo wakaanzishe viwanda vidogo vidogo vitakavyo changia ukuaji wa pato la Taifa .
Sambamba na hayo Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Dkt. Maulid Madeni naye akizungumza katika mafunzo hayo alimwambia Mgeni Rasmi kuwa Halmashauri itaendelea kutoa mikopo hiyo ikiwa ni kuendelea kutekeleza ilani ya Chama Cha Mapinduzi, pia alieleza changamoto kubwa zinazojitokeza ni utengengenezaji wa vikundi hewa wakati wa utoaji mikopo, ucheleweshwaji wa marejesho na maranyingine marejesho ya fedha hizo za mikopo kupokelewa na watu wasio stahili hali inayopelekea fedha hizo kutofikishwa mahali husika. Vilevile alitoa onyo kwa wanaounda vikundi hewa na kuwaamuru waache vitendo hivyo na kuelekeza kuwa marejesho ya fedha za mikopo yapokelewe na wahusika lakini pia stakabadhi za marejesho zihifadhiwe kwa umakini. Dkt. Madeni alimshukuru Mhe. Rais wa Jamuhuri wa Muungano waTanzania Dkt. Joh Pombe Joseph Magufuli kwa kutoa fedha hizo kwa Wananchi zitakazo wawezesha kutatua matatizo yao na kuwakuza kiuchumi na kukuza pato la Taifa.
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa