Halmashauri ya Jiji la Arusha imekuwa ikipokea wageni kutoka miji mbali mbali ndani na nje ya nchi kwa ajili ya kujifunza mambo mbalimbali ya kiutendaji .
Mnamo Tarehe 16/10/2017 Halmashuuri ya Jiji la Arusha ilipokea wageni (Naibu Meya, Mkurugenzi, Madiwani na baadhi ya Watendaji) kutoka Manispaa ya Bukoba ambapo lengo kuu la ziara yao lilikuwa ni kujifunza juu ya mfumo wa usimamizi wa ukusanyaji wa mapato, usimamizi wa uzoaji taka na utekelezaji wa miradi ya uboreshaji miji na majiji inayofadhiliwa na benki ya dunia (ULGSP na TSCP).
Pamoja na ziraya yao ya kimafunzo pia walipata fursa ya kutembelea eneo la machinjio ya kisasa yanayomilikiwa na Halmashauri ya Jiji la Arusha (Arusha Meat) na kujionea namna yanavyofanya kazi kwa usafi na ufanisi wa hali ya juu.
Pia walipata fursa ya kutembelea bustani inayoishi ya Themi (Themi Living Garden) ambayo katika historia hapo mwanzo ilikuwa kichaka cha wahalifu ila baadae Halmashuri ya Jiji la Arusha iliamua kuhifadhi eneo hilo na kuwa mahala pa mapumziko. Kwa sasa linasimamiwa na kampuni ya watu wa Itali, Oikos baada ya kuingia nao mkataba wa maridhiano juu ya utunzaji wa mazingira.
Aidha Halmashauri ya Jiji la Arusha Tarehe 19/12/2017 pia ilipokea Madiwani 42, Wakuu wa Idara 9 na Wataalam watano kutoka Manispaa ya Morogoro kujifunza Uthamini wa Mali za Halmashauri.
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa