Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha Dkt. John Pima amewaasa viongozi wote wa ngazi za Kata mpaka mitaa wa Halmashauri ya Jiji hilo kujitokeza kwa wingi kupata Chanjo ya UVIKO-19 ili kuwa mfano katika jamii inayowazunguka na hivyo kuwahamasisha wananchi wengine kupata Chanjo.
Dkt. Pima ameyasema hayo leo alipokuwa akiongea na viongozi hao katika kikao chenye lengo la kuhamasisha wananchi kupata Chanjo ya UVIKO-19 kilichofanyika katika Ukumbi wa Ofisi za Kata ya Oloirieni, iliyopo Jijini Arusha.
Kimsingi Dkt. Pima amewasisitiza viongozi hao kuwa mabalozi wazuri juu ya chanjo ya UVIKO-19 na kuongeza kuwa chanjo hiyo ni salama kwani kwa kufanya hivyo wataokoa maisha yao na ya wananchi wanaowahudumia.
Dkt. Pima ameongeza kuwa chanjo hiyo ni salama na kwamba wananchi wajitokeze kwa wingi ili kuweza kuwa salama wao na familia zao.
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Halmashauri Jiji la Arusha Dkt. Nindwa Maduhu amesema lengo kubwa la kuhamasisha zoezi hilo ni kuweza kuifanya Tanzania kufikia Kinga Jamii ambayo ni asilimia 80 ya watu wote watakaokuwa wamechanja na kwamba wataweza kufanikisha zoezi hilo kwa kuwafikia na kuwashirikisha wananchi wa ngazi za chini kwani kwa kufanya hivyo kuwahamasisha watu wengi kuchanja na hivyo kuwa salama.
Naye Diwani wa kata ya Olorieni Mhe. Lawrence Kombe ameishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Rais Samia Suhulu Hassan kwa kuwajali wananchi wake kwa kuleta chanjo hiyo na kuwasisitiza wananchi kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa huo kwa kuchanja kwani kufanya hivyo kuwasaidia kuokoa maisha yao.
Bw. Thomas Msaka mmoja wa wananchi waliopata chanjo, amesema viongozi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha kusogeza huduma hiyo kwa ngazi za chini za kata na mitaa kutawafanya wananchi wengi kujitokeza kwa wingi kupata Chanjo hiyo.
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa