Halmashauri ya jiji la arusha imekuwa ikipokea wageni kutoka miji mbalimbali nchini na nje ya nchi kwa ajili ya kujifunza mambo mbalimbali ya kiutendaji.
Jana tarehe 18/07/2019 Halmashauri ya jiji la Arusha ilipokea wataalamu 30 kutoka kisumu nchini kenya ambapo lengo kuu la ziara yao ilikuwa ni kujifunza juu mfumo wa usimamizi na uendeshaji wa Jaa la kisasa lililopo murriet sambamba na mifumo ya maji na uhifadhi wa mazingira,mfumo wa usimamizi na ukusanyaji wa mapato pamoja na namna Jiji la Arusha linavyoendesha na kuongoza shughuli zake.
Sambamba na ziara hiyo wageni walipata fursa ya kutembelea maeneo mbali mbali ya Jiji la Arusha ikiwemo eneo lilipo Jaa hilo na kujionea shughuli zinavyoendeshwa kwa ufanisi na usimamizi mzuri.
Ugeni huo kutoka kenya uliambatana na mkurugenzi wa Jiji la kisumu pamoja na wakuu wa idara za jiji hilo pamoja na mwenyekiti na wanachama wa bodi ya jiji la Kisumu.
Wageni hao kutoka Kisumu nchini Kenya pia walifurahia mapokezi na ukarimu wa watanzania pamoja na mafunzo maridhawa kutoka kwa wataalamu wa halmashauri ya Jiji la Arusha waliobobea katika fani zao akiwemo Kaimu mhasibu wa mapato Jiji la Arusha,Afisa usafishaji na mazingira Jiji la Arusha,Kaimu mwanasheria, Afisa maliasili na utalii pamoja na kaimu mhandisi wa jiji.
"Pichani: Afisa usafishaji na mazingira Bw. James Lobikoki akitoa mafunzo kwa wageni kutoka Jiji la Kisumu"
******************************************************
"Pichani: Kaimu mhasibu wa mapato Jiji la Arusha Bi. Felista Kitambi akitoa mafunzo kwa wageni kutoka Kisumu"
***************************************************
"Pichani: Afisa maliasili Bw.Michael Ndaisaba akitoa mafunzo kwa wageni kutoka Kisumu"
**************************************
"Pichani: Moja kati ya miradi inayoendelea ya uboreshaji wa Jaa la Murriet"
“UDUMU URAFIKI WA KENYA NA TANZANIA”
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa