Halmashauri ya Jiji la Arusha imesaini Mkataba wa makubaliano na Taasisi ya OIKOS Tanzania kutekeleza mradi wa TERRA wenye malengo ya kuelimisha jamii juu ya athari za mabadiliko ya Tabia ya Nchi na namna ambavyo wanaweza kukabiliana na maadiliko hayo.
Akizunguma wakati wa kusaini Mkataba huo wa makubaliano Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Athumani Kihamia amesema kupitia mradi huu Arusha itakua na uhalisia wa kuitwa “Geneva of Africa” kwa sababu muonekano wa Jiji hili baada ya mradi huu utavutia zaidi, mazingira yatakuwa bora na wananchi haswa wakulima na wafugaji watafanya shughuli zao katika eneo salama.
“Tunashukuru sana kupata mradi huu wa kipekee kwa kuwa tumekuwa tukipata miradi mingi ya maendeleo katika sekta za Miundombinu, Elimu, Afya, Kilimo na Mifugo lakini huu tunaosaini sasa utasaidia sana kwenye suala zima la Mazingira katika dhana ya mabadiliko ya Tabia ya Nchi” alisema Kihamia.
Aliongeza kuwa atahakikisha wanachi wake wanashirikiana begabega na wasimamizi wa mradi huo katika kuhakikisha mradi huo unatekelezeka ili kujiletea maendeleo binafsi na ya Taifa kwa ujumla.
Mkurugenzi wa OIKOS Afrika Mashariki Mhe. Ramadhan Kupaza amesema Jiji la Arusha ni eneo ambalo wamefanikiwa sana katika miradi iliyopita hivyo wameona ni vyema wakatekeleza mradi huu hapa ili uweze kuboresha zaidi miradi iliyopita na kuweza kuwa na Tija zaidi kwa jamii.
Aliongea kuwa mradi huu utatekelezwa kwa kipindi cha miaka mitatu na utawezesha zaidi ya familia 6,000 za kifugaji kuweza kupata suluhisho la kudumu juu ya madhara yatokanayo na mabadiliko ya hali ya hewa ambapo utaangazia hasa juu ya utunzaji wa ardhi, njia mbadala za vyanzo vya nishati, kilimo kinachozingatia majira ya nchi.
Pia utaongeza Mradi huu utasaidia kuongeza Tija katika bidhaa za kilimo na Mifugo kama vile kujenga viwanda kutengeneza bidhaa zinazotokana na Ngozi za wanyama na kuwawezesha wananchi kuhifadhi maeneo ya malisho ya mifungo kwa ajili ya usalama wa Mifugo yao.
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa