Jiji la Arusha kufungwa taa za Barabarani ili kuongeza usalama wa wananchi na mali zao katika maeneo yao.
Hayo yamebainishwa na Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha Maximilian Iranqhe ambae pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya fedha ya Halmashauri ya Jiji la Arusha ilipokuwa ikifanya ukaguzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo.
Mstahiki Meya amesema kutokana na Jiji la Arusha kuwa la kitalii ni muhimu taa za Barabarani kuwepo ili watalii wawekatika mazingira salama zaidi.
Amesema kufungwa kwa taa hizo kutaongeza usalama kwa watumiaji barabara hizo.
Mradi huo umeshaanza kwa kuweka taa katika barabara Simeon,Somali,East Afrika, Makongoro Ingira,Wachaga,Sokoine, Kanisa na Stend Kuu.
Nae, Kaimu Mkurugenzi Halmashauri ya Jiji la Arusha Dkt. Onesmo Mandike amesema Halmashauri imetoa zaidi ya Milioni 800 kwa ajili ya ununuzi wa taa 255.
Dkt. Mandike amesema Halmashauri ilitenga kiasi cha bilioni 1 kwa ajili ya uboreshaji wa miundombinu ya taa za barabarani katika mwaka wa fedha 2022/2023 na halmashauri inaendelea kutenga fedha hizo kila mwaka.
Kamati ya Fedha ya Halmashauri ya Jiji la Arusha imekagua miradi mbalimbali ikiwepo uwekaji wa taa za Barabarani na katika baadhi ya shule, Bustani ya Miti ya Halmashauri hiyo, ufugaji wa Samaki, standi ya Daladala ya Themi,Vijiwe vya Kahawa na Dampo la takataka ikiwa ni ufanyaji wa tathimini katika robo ya kwanza ya mwaka 2023/2024.
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa