Halmashauri ya Jiji la Arusha imetia saini mkataba mpya na kampuni ya Sinohydro Co-Operation Ltd ya nchini China kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa uboreshaji Miji na Majiji nchini (TSP) awamu ya tatu wenye gharama ya sh. Bilioni 22. 3 katika ofisi za makao makuu ya Jiji.
Mradi huo utajumuisha ujenzi wa barabara za lami za ndani katika Jiji la Arusha, bwawa la kuhifadhia taka ngumu pamojana uwanja wa mpira wa shule ya msingi Ngarenaro.
Akizungumza katika ghafla hiyo ya utiaji saini Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo alitaja barabara hizo kuwa ni Oljoro-Murriet, Njiro km 2.5, soko la Krokon km 0.64, Ngarenaro km 4.3 na Sombetini km 1.85
Gambo alimtaka mkandarasi huyo kutekeleza mradi huo kwa wakati ili kuwaondolea adha wananchi wanaotumia barabara hizo ambazo zimekuwa na changamoto kubwa hususan nyakati za mvua ambapo maji hujaa katika nyumba zao.
“Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Ndg. Athumani Kihamia ametujulisha kuwa mkataba unasema mradi huu utatekelezwa kwa muda wa miezi 15. Mkandarasi nakuagiza utekeleze mradi huu kwa wakati na mradi huu hamjapewa kwa upendeleo wala kuonewa huruma ni kutokana na sifa pamoja na kukidhi vigezo hivyo msitishwe na wanasiasa wakati wa kutekeleza mradi huu” alisema MKUU wa Mkoa.
Naye mkurugenzi wa Jiji la Arusha alisema kuwa upembuzi yakinifu wa mradi umeshakamilika na ofisi yake imeshalipia fidia ya sh. Milioni 250 kwa wananchi ambao nyumba zao zimepitiwa na barabara.
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa