• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Arusha City Council
Arusha City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Fedha na biashara
      • Utumishi na Utawala
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Afya
      • Mifugo na Uvuvi
      • Primary Education
      • Elimu Sekondari
      • Usafishaji na Mazingira
      • Works and Infrastucture
      • Water
      • Mipango, Uchumi na takwimu
      • Mipango miji
      • Maendeleo na Ustawi wa Jamii
    • Vitengo
      • Sheria
      • Tekinolojia ya habari Mawasiliano na Mahusiano
      • Manunuzi
      • Internal Audit
      • Uchaguzi
      • Ufugaji wa nyuki
    • Kata
      • Baraa
      • Daraja II
      • Elerai
      • Engutoto
      • Kaloleni
      • Kati
      • Kimandolu
      • Lemara
      • Levolosi
      • Moivaro
      • Moshono
      • Murriet
      • Ngarenaro
      • Olasiti
      • Olmoti
      • Oloirien
      • Osunyai
      • Sakina
      • Sekei
      • Sinon
      • Sokon I
      • Sombetini
      • Terrat
      • Themi
      • Unga Ltd
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Usafi wa Mazingira
    • Elimu
    • Biashara
    • Maendeleo ya Jamii
    • Leseni
  • Madiwani
    • Orodha ya Wahe.Wabunge na Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Maadili
      • Kudhibiti UKIMWI
    • Ratiba
      • Ratiba za Vikao
      • Ratiba ya kumuona Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu za Maombi
    • Mkataba wa huduma kwa wateja
    • STUDY ONLINE
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Hotuba
    • Taarifa kwa umma

Jiji la Arusha laendelea kuwajali wamachinga, Meya Iranqhe ahimiza ushirikiano.

Posted on: May 21st, 2023

Na Mwandishi Wetu 

Arusha 

Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha Mhe. Maximilian Matle Iranqhe amewataka wafanyabiashara wadogo maarufu Kama Machinga Jijini Arusha  kuiamini Serikali kwakua inawajali na kuwatatulia changamoto zinazowakabili ikiwemo miundombinu ya masoko na kwa kuanza wameshamwaga na kusambaza moramu katika baadhi ya masoko kama Machame Luxury, Namba 68, Soko la Kilombero, Samunge na mengineyo. 


Mhe. Iraqhe alitoa wito huo Mei 21, 2023 wakati alipotembelea na kukutana tena na machinga hao katika soko la Machame Luxury  lililopo Jijini Arusha kwa lengo la kufuatilia na kushuhudia utekelezaji wa ahadi ya utatuzi wa changamoto zinazowakabili machinga ambazo Meya Iranqhe aliahidi kuzifanyia kazi wiki mbili zilizopita alipotembelea masoko hayo. 


Pia, alimwomba Mwenyekiti wa Soko hilo kuwaunganisha pamoja wafanyabiashara wa soko hilo na asiruhusu mtu yeyote kuwagawa wamachinga hao  pamoja na kushirikiana na Serikali nakuongeza kuwa yale yote walioahidiwa watatekelezewa. 


"Niwaombe muiamini Serikali yenu, niwaombe muwaamini viongozi wa wamachinga kwenye soko hili lakini machinga Wilaya lakini pia mumuamini Mkuu wenu wa Wilaya, Mbunge, Mkuu wa Mkoa, Mkurugenzi hawa wote wanafanyakazi chini ya ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kwa hiyo wote tunajenga nyumba moja tusigombalnie fito " alisema Iranqhe. 


Aidha, alibainisha kuwa wanataka Jiji la Arusha liwe Jiji la kwanza  kwa kujiendesha lenyewe kwa mapato  ya ndani ndio maana Serikali inajenga masoko ya kimkakati. 


"Ninaomba kila mtu aamini Serikali tuko hapa kwa ajili ya  kutatua matatizo yenu kutatua changamoto zenu  na kuhakikisha maisha yenu yanapanda maana yake ukiwa kijana unaweza kuwa machinga hapa na pale lakini ukiwa mtu mzima huwezi kuwa machinga Sasa lengo la Serikali  nikuwaanda kutoka kwenye umachinga kwenda kwenye wafanyabiashara wa kati, wafanyabiashara wakubwa na mimi naamini hii inawezekana tukishirikiana kwa pamoja " alisema Meya Iranqhe. 


Aidha aliongeza kuwa katika asilimia kumi ya mikopo inayotolewa na Halmashauri ya Jiji la Arusha  Wanataka kuwapatia mikopo wamachinga ili watoke kwenye umachinga na kwenda kuwa wafanyabiashara. 


Kwa upande wake kiongozi wa machinga Wilaya ya Arusha, Idrisa Chongoza aliishukuru Serikali na viongozi wa Jiji hilo akiwemo Mstahiki Meya na Mkurugenzi wa wa Jiji hilo  kwa kuwatatulia changamoto zinazowakabili ikiwemo uboreshaji wa miundombinu ya masoko.


"Nawaombeni sana wafanyabiashara wenzangu tulieni kwa sababu Serikali inapokuja kutekeleza majukumu yake ikiwakosa tena eti mko barabarani mnahangaika hasa itakuwa inamtengenezea nani sisi wafanyabiashara tujikague wenyewe tukae Sasa kwenye maeneo yetu ya biashara tuhakikishe tunatulia  Serikali imeshaanza kufanyakazi Arusha yetu itatulia maisha yataendelea " Alisema Chongoza.

Matangazo

  • NAMNA YA KUPATA KIBALI CHA KUSAFIRI NJE YA NCHI KWA WATUMISHI WA SERIKALI January 16, 2025
  • MATOKEO YA USAILI WA MCHUJO KADA YA MTENDAJI WA MTAA NA KADA YA MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU October 06, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI October 15, 2024
  • TANGAZO LA MIKOPO October 29, 2024
  • Tazama zote

Habari za hivi punde

  • JIJI LA ARUSHA LAZINDUA MITAMBO MIPYA

    January 28, 2025
  • MKURUGENZI KAYOMBO AKABIDHIWA OFISI

    August 21, 2024
  • WANAWAKE NA WASICHANA KUJENGEWA UWEZO WA KISHIRIKI NAFASI ZA UONGOZI

    August 20, 2024
  • NENDENI MKAONGEZE UFANISI

    August 19, 2024
  • Tazama zote

Video

JIUNGE NA MFUMO WA TAUSI
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • MIRADI ILIYOKAMILIKA
  • MKATABA WA HUDUMA KWA WATEJA
  • SISI NI NANI
  • Urban Sanitation and Hygiene | Mazingira safi Maisha bora

Viunganishi Linganifu

  • TAMISEMI
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Utumishi
  • Tovuti ya ajira
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Counter

Location Map

Wasiliana nasi

    20 Boma Street 23101

    Sanduku la Posta: 3013

    Simu: 0272548072

    Simu ya Mkononi: 0272545768

    Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa