Shirika la Bima la Taifa Tanzania (NIC) latoa msaada wa mabati 300 jana tarehe 19/07/2019 yenye thamani ya kiasi cha fedha shilingi milioni nane na laki moja za kitanzania. Akiongea mkurugenzi mtendaji wa shirika hilo Ndg. Sam Kamanga alisema shirika la bima ya taifa limetoa msaada wa mabati hayo kwa Wilaya za mkoa wa Arusha ikiwa ni moja kati ya misingi ya utawala bora ambayo serekali inahimiza . “shirika la bima la taifa lina wataalamu ambao wote ni wazawa na wazalendo kwa hiyo tunaona kwamba kuna umuhimu wa aina yake kufika mahali shirika likatoa huduma kwa jamii na sio kufanya biashara tuu” alizungumza mkurugenzi mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa Tanzania (NIC).
Sambamba na hayo vilevile mkurugenzi mtendaji wa shirika la Bima la Taifa Tanzania Ndg. Sam Kamanga ameahidi ya kuwa mara hii ni mara ya kwanza shirika hilo likitoa masaada kwa mkoa wa Arusha hivyo haitakuwa mara mwisho watajitahidi kwa kadiri wapatavyo kuendelea kutoa huduma kwa wananchi.
Akipokea msaada huo wa mabati Mkuu wa wilaya ya Arusha Mhe. Gabriel Daqarro amelishukuru Shirika la Bima la Taifa Tanzania(NIC),mkurugenzi mtendaji pamoja na meneja wa mkoa wa shirika la bima la taifa kwa msaada huo akisema serekali chini ya uongozi wa Mhe. Rais Dkt John Pombe Magufuli inatoa elimu bila malipo hivyo kumekuwa na msongamano na muitikio chanya wa wazazi kuleta watoto shule kuanzia ngazi ya msingi hadi sekondari hivyo tunashukuru Shirika la Bima la Taifa Tanzania (NIC) kwa kuunga mkono juhudi na jitihada za kuhakikisha kila mototo wa kitanzania anapata elimu iliyo bora.
Mkurugenzi wa jiji la Arusha Dkt. Maulid Suleiman Madeni naye amemshukuru Mkuu wa wilaya ya Arusha Ndg. Gabriel Daqarro kwa juhudi za kuongea na wadau na kuweza kulisaidia Jiji la Arusha kutekeleza ilani ya uchaguzi ya Chama cha mapinduzi (CCM) ya mwaka 2015 inayo sisitiza elimu bure hivyo kumuwakilisha vizuri Mhe. Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli. “vilevile nashukuru Shirika la Bima la Taifa Tanzania(NIC) kwa mchango wao mahiri kabisa na mchango wao mzuri wakizalendo wakujali maslahi ya wengi” alisema mkurugenzi wa Jiji la Arusha Dkt. Maulid Suleiman Madeni.
Pichani: Mkuu wa wilaya ya Arusha Ndg. Gabriel Daqarro na Mkuregenzi wa Jiji la Arusha Dkt. Maulid Suleiman Madeni wakipokea msaada wa mabati kutoka Shirika la Bima la Taifa Tanzania(NIC)
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa