Na Mwandishi Wetu.
Arusha Jiji.
Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe. Felician Mtahengerwa,amepongeza jitihada za Jiji la Arusha kuhakikisha makundi hayo yanawezeshwa na kujikwamua kiuchumi na haijawahi kutokea Halmashauri kutoa kiasi kikubwa cha fedha namna hiyo.
Amesema kuwa, mikopo hiyo ina nia njema ya kuwakomboa wananchi wake kutoka kwenye hali duni zaidi ili waweze kufanya biashara na kujikwamua kiuchumi.
"Nawaomba sana mkafanye biashara zenye ubunifu ili muweze kurejesha kwa wakati na wenzenu wengine waweze kupata na hata kuiga mfano kutoka kwenu kwani itawasaidia kutoka sehemu moja kwenda nyingine" amesema Mtahengerwa.
Naye Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha Mhe. Maximilian Matle Iraqhe amesema kuwa kwa mara ya kwanza Jiji la Arusha limevunja rekodi ya kutoa pesa nyingi kupitia mapato ya fedha za ndani .
Amesema kuwa Jiji la Arusha makisio ya ukusanyaji wa mapato yameongezeka kutoka Tsh. 30.5 bilioni kwa mwaka wa fedha 2022/2023 hadi kufikia Tsh. 60.6 bilioni kwa mwaka 2023/2024 sawa na ongezeko la asilimia 100 .
"Kupitia fedha hizi zilizotolewa leo tunatarajia kuwa na jiji la Arusha litabadilika na vijana kuweza kujikwamua kiuchumi kwa kujihusisha na shughuli mbalimbali na hatimaye kuweza kutengeneza ajira kwa vijana wengine."amesema Iraghe.
Kaimu Mkurugenzi Jiji la Arusha Bw. Hargeney Chitukuro amesema kuwa,Halmashauri hiyo imekabidhi hundi ya Shilingi 2.6 bilioni kwa vikundi 169 vya wanawake ,vijana na watu wenye walemavu.
Amesema kuwa jumla ya vikundi 205 viliwasilisha maombi yao kwenye mfumo wa TPL-MIS, ambapo uhakiki ulifanyika na kubaini kuwa vikundi 7 vimejikita katika shughuli zenye mwelekeo wa uzalishaji kupitia vikundi vidogovidogo na usindikaji.
Aidha amesema kuwa, vikundi 28 vinafanya miradi ya uzafirishaji ,77 vinajihusisha na miradi ya kilimo na ufugaji,na vikundi 93 vinajihusisha na biashara na ujasiriamali ambapo katika hivyo vikundi 169 ndivyo vilivyokidhi vigezo.
Aidha amesema kuwa, Halmashauri ya Jiji la Arusha kuanzia julai hadi sasa hivi walishatoa kiasi cha shs 3. 9 bilioni kwa vikundi 339 hadi sasa hivi ambapo zimewawezesha kutengeneza ajira mbalimbali kwa makundi hayo.
Amesema kuwa,kati ya vikundi hivyo jumla ya vikundi 127 ni vya wanawake,huku vikundi vya vijana vikiwa 32,na watu wenye ulemavu vikiwa 10 .
"Haijawahi kutokea Jiji la Arusha kutoa mikopo ya fedha nyingi hivi,hivyo tunawaomba sana mnaopatiwa mikopo hii leo mkawe warejeshaji wazuri na mkarejeshe kwa wakati ili na wenzenu waweze kunufaika kupitia mikopo hiyo na kujikwamua kiuchumi."amesema .
#arusha #tanzania #KaziIendelee
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa