• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Arusha City Council
Arusha City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Fedha na biashara
      • Utumishi na Utawala
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Afya
      • Mifugo na Uvuvi
      • Primary Education
      • Elimu Sekondari
      • Usafishaji na Mazingira
      • Works and Infrastucture
      • Water
      • Mipango, Uchumi na takwimu
      • Mipango miji
      • Maendeleo na Ustawi wa Jamii
    • Vitengo
      • Sheria
      • Tekinolojia ya habari Mawasiliano na Mahusiano
      • Manunuzi
      • Internal Audit
      • Uchaguzi
      • Ufugaji wa nyuki
    • Kata
      • Baraa
      • Daraja II
      • Elerai
      • Engutoto
      • Kaloleni
      • Kati
      • Kimandolu
      • Lemara
      • Levolosi
      • Moivaro
      • Moshono
      • Murriet
      • Ngarenaro
      • Olasiti
      • Olmoti
      • Oloirien
      • Osunyai
      • Sakina
      • Sekei
      • Sinon
      • Sokon I
      • Sombetini
      • Terrat
      • Themi
      • Unga Ltd
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Usafi wa Mazingira
    • Elimu
    • Biashara
    • Maendeleo ya Jamii
    • Leseni
  • Madiwani
    • Orodha ya Wahe.Wabunge na Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Maadili
      • Kudhibiti UKIMWI
    • Ratiba
      • Ratiba za Vikao
      • Ratiba ya kumuona Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu za Maombi
    • Mkataba wa huduma kwa wateja
    • STUDY ONLINE
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Hotuba
    • Taarifa kwa umma

Jiji la Tanga laimwagia sifa Jiji la Arusha

Posted on: February 23rd, 2022

Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga, Abdurahman Shiloow


Na Mwandishi,

Arusha.

Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Abdurahman Shiloow amelimwagia sifa jiji la Arusha kwa utekelezaji wa miradi mingi na mikubwa ya maendeleo pamoja na ushirikiano mzuri uliopo kati ya ofisi ya Mkurugenzi, Mstahiki Meya pamoja ofisi ya Mkuu wa wilaya.

Mhe. Shiloow ameyasema hayo leo kwenye Mkutano wa Baraza la Madiwani robo ya pili ya mwaka 2022 ambapo madiwani na wataalam kutoka Jiji la Tanga walikuwa kwenye ziara ya kutembelea miradi ya maendeleo inayotekelezwa na jiji la Arusha.

“Hapa Arusha tuna mengi ya kujifunza, kuanzia miradi mlionayo, uhusiano mzuri kati ya Mkurugenzi, madiwani na Mkuu wa wilaya, lakini kingine ni matumizi ya teknolojia kwa maana ya Kishkwambi, naona kila diwani na wataalamu wa hapa Jiji la Arusha mnatumia Kishkwambi, haya ni mambo muhimu kwetu kuyaiga” Alisema Mhe. Shiloow.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe. Said Mtanda aliwakaribisha madiwani hao kutoka Tanga na kuwataka kuendelea kutembelea jiji la Arusha ili kujifunza zaidi na kusema siri kubwa ya maendeleo hayo ni uwepo kwa utulivu wa kisiasa miongomi mwao.

Mhe. Mtanda aliwataka madiwani wa Jiji la Arusha kuendeleza utulivu na umoja uliopo ili kuhakikisha maendeleo yanapatikana kwani migogoro huchelewesha maendeleo kwa wananchi.  Ambapo alisema

“Haya yote yanatokana na utulivu uliopo kwani maendeleo hayataki kelele, kwa hiyo tuendelee kuheshimiana ili kuhakikisha jiji letu linaendelea kuwa mfano wa kuigwa nchini na kubwa zaidi wananchi wetu wapate huduma bora kama serikali ilivyokusudia”

Katika upande wa elimu na mapato, Mkuu wa Wilaya amesema jiji la Arusha linaendelea kuongoza kwani katika matokeo ya darasa la saba kwa shule za serikali, jiji la Arusha limeendelea kuongoza kwa kushika nafasi nne kitaifa mfululizo na katika ukusanyaji mapato awali lilishika nafasi ya kwanza na sasa limeshika nafasi ya pili kitaifa.

Madiwani kutoka jiji la Tanga katika kipindi cha uwepo wao watatembelea miradi mbalimbali iliyopo Jiji la Arusha ikiwemo madarasa ya ghorofa katika shule ya sekondari Arusha Terrat, pamoja na shule ya sekondari Unga Ltd, mradi wa matofali uliopo eneo la Njiro pamoja na miradi ya maeneo ya wazi ya uwekezaji  wa vivutio vya utalii Themi Living Garden.

Miradi mingine watakayotembelea ni soko la Machinga kiwanja Na. 68 ulilopo eneo la Kilombero, maduka ya biashara Krokon na Ranger Safari pamoja na eneo la wazi la Levolosi ambapo miradi yote imejengwa kwa fedha za mapato ya ndani za Halmashauri ya Jiji la Arusha.


Matangazo

  • NAMNA YA KUPATA KIBALI CHA KUSAFIRI NJE YA NCHI KWA WATUMISHI WA SERIKALI January 16, 2025
  • MATOKEO YA USAILI WA MCHUJO KADA YA MTENDAJI WA MTAA NA KADA YA MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU October 06, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI October 15, 2024
  • TANGAZO LA MIKOPO October 29, 2024
  • Tazama zote

Habari za hivi punde

  • JIJI LA ARUSHA LAZINDUA MITAMBO MIPYA

    January 28, 2025
  • MKURUGENZI KAYOMBO AKABIDHIWA OFISI

    August 21, 2024
  • WANAWAKE NA WASICHANA KUJENGEWA UWEZO WA KISHIRIKI NAFASI ZA UONGOZI

    August 20, 2024
  • NENDENI MKAONGEZE UFANISI

    August 19, 2024
  • Tazama zote

Video

JIUNGE NA MFUMO WA TAUSI
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • MIRADI ILIYOKAMILIKA
  • MKATABA WA HUDUMA KWA WATEJA
  • SISI NI NANI
  • Urban Sanitation and Hygiene | Mazingira safi Maisha bora

Viunganishi Linganifu

  • TAMISEMI
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Utumishi
  • Tovuti ya ajira
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Counter

Location Map

Wasiliana nasi

    20 Boma Street 23101

    Sanduku la Posta: 3013

    Simu: 0272548072

    Simu ya Mkononi: 0272545768

    Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa