WAJUMBE wa kamati ya Fedha na Utawala ya Halmashauri ya Jiji la Arusha wametembelea miradi saba ya Jiji hilo na kuleta matumaini Kwa wananchi ikiwa ni pamoja na kuahidi utekelelezaji wa miradi hiyo.
Miradi iliyotembelewa ni pamoja na uanzishwaji wa masoko ambayo yapo kwenye mipango ya uboreshaji wa ukusanyaji wa mapato ya Jiji la Arusha.
Miradi ya masoko iliyotembelewa na kukaguliwa ni pamoja Kata Baraa soko baraa, Kata ya Muriet soko la Nadosoito, Soko la samunge na soko la mbauda.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha Mhe. Maxmillian Iranqhe amesema lengo la zoezi hilo ni kuboresha mapato ya Halmashauri hatimaye kuwaletea wananchi maendeleo.
Aidha Amewahakikishia kuwa masoko hayo yataanza kutumika haraka iwezekanavyo kwa kuwa yapo kwenye mipango ya maendeleo ya Jiji la Arusha.
Pamoja na mambo mengine amewataka kuhakikisha kuwa maeneo ya masoko yenye migogoro akitolea mfano soko la Nadosoito ametaka migogoro kutafutiwa ufumbuzi kwa kuwa serikali haiwekezi katika maeneo yenye migogoro na kwamba punde tu migogoro hiyo itakapotatulika serikali itaruhusu uwekezaji maeneo hayo.
Naye, Diwani wa kata ya Muriet akizungumza kwa niaba ya wananchi wa Kata hiyo amemuhakikishia Meya wa Jiji la Arusha kuwa mgogoro uliopo katika eneo la soko hilo upo kwenye hatua za mwisho za utatuzi na kwamba watampelekea taarifa za utatuzi wa mgogoro huo na hatimaye ujenzi wa soko uendelee.
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa