Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Mashaka Gambo amepokea vifaa tiba kutoka kampuni ya mawasiliano Vodacom kwaajili ya kituo cha Afya Murriet leo Tarehe 27/05/2020.
Kampuni hiyo imetoa msaada wa vifaa tiba vyenye thamani ya shilingi 42,621,600 fedha za kitanzania. Vifaa hivyo vikiwa ni vifaa vya Oxygen kwaajili ya kuwezesha watoto kupumua, viongeza joto kwaajili ya kusaidia kuhifadhi watoto njiti, mashine za tiba mwanga na mashine maalumu kwaajili ya kupima mapigo ya moyo ya mtoto.
Sambamba na hayo Mhe. Gambo amefanya ukaguzi wa baadhi ya majengo ya kituo hicho cha afya na kuridhishwa na hatua zilizofikiwa za ukamilishaji wa majengo hayo ili kuanza kutoa huduma siku za usoni. Majengo hayo ni pamoja na jengo la kuhifadhi maiti, maabara, jengo la mionzi (X-Ray) pamoja na jengo la upasuaji.
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa