Halmashauri ya jiji la Arusha limezindua kanuni mpya za kuduma zitakazoongoza uendeshaji wa vikao vya Kamati pamoja na Baraza la Madiwani la Jiji la Arusha kuanzia mwaka ujao wa Fedha 2017/2018.
Uzinduzi huo umefanyika katika kikao cha kota ya Nnne cha Baraza la Madiwani kilichoketi mapema mwezi Julai kupitisha taarifa za utendaji kazi wa Halmashauri kwa kipindi cha mwaka mzima wa 2016/2017.
Akifungua kikao hicho Mstahiki Meya wa jiji la Arusha Mhe. Kalisti Lazaro Bukhay alisema ni muhimu kwa kila diwani kuzisoma na kuzifahamu kwa undani Kanuni hizo za kudumu na kuzizingatia katika kila kikao ili kupesha mkakanganyiko uliokuwa unatokea hapo awali wakati wa uendeshaji wa vikao.
“Haiwezekani Mhe.Diwani unachangia hoja moja zaidi ya dakika 20 au Diwani mwingine anarudia hoja ambayo mjumbe wa awali alikwisha izungumza hapo awali kirefu na na kusababisha kikao kimoja kufanyika kwa siku nzima bila kukamilika hii kusababisha upotevu wa muda na rasimaliza za Halmashauri”.
Aliongea kuwa katika mwaka ujao wa Fedha anategemea ukomavu wa madiwani na wataalamu katika uendeshaji na usimamzi wa Vikao na hategemei kushuhudia makosa madogo madogo kama yale yaliokuwa yakijitokeza katika vikao vinavyoishia katika mwaka huu wa fedha.
Sambamba na hilo Mkurugenzi wa Jiji Ndg. Athuman kihamia ameelezea mafanikio ya Jiji yaliyopatikana kwa kipindi cha mwaka husika kuwa ni pamoja suala la ukusanyaji wa Mapato kwani wamevuka malengo kwa zaidi ya asilimi 13.
“Kwa mara ya kwanza katika historia ya Jiji tumekusanya Mapato ya ndani kwa asilimia 113 na kuweza kuchangia asilimia 60 ya mapato hayo kutekeleza shughuli za maendeleo huku asilimia 40 ikitumika katika matumizi mengine ikiwemo mishahara ya watumishi na kuendesha ofisi” alisema Kihamia.
Sambamba na hilo mafanikio mengine yamepatikana katika uboreshaji wa miundombinu kazi kubwa iliyofanyika ni ujenzi wa barabara kwa kiwango cha Lami, changarawe, matengenezo ya muda maalum, vivuko pamoja na madaraja katika baadhi ya barabara.
Aliongea kuwa “tulifanikiwa zaidi katika ujenzi na ukarabati wa vyumba vya madarasa 87 kwa shule za msingi na sekondari na pamoja na ujenzi wa vituo vitano vya kutolea huduma za afya ambavyo vipo katika hatua mbalimbali za ukamilishaji.
Aidha Kikao hicho cha baraza la madiwani kiliweza kupokea taarifa mbalimbali kutoka katika Taasisi za kiserikali zinazotoa huduma kwa wananchi wa jiji la ArushA kufanya uchaguzi wa wenyeviti wa Kamati za Kudumu pamoja wajumbe sanjari na uchaguzi wa Naibu Meya wa Jiji la Arusha.
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa