Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Ndg. Athumani Kihamia amedhihirisha umahiri wake kiutendaji kwa kuongoza mafuzo ya wabunge wawili, Wah. Madiwani 35 na wataalamu watano (5) kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero waliofanya ziara ya kimafunzo katika Halmashauri ya jiji la Arusha.
Kihamia ametoa upendeleo huo na heshima kubwa kwa ugeni huo mapema hapo juzi ambapo Lengo la ziara ya wataalamu hao lilikuwa ni kujifunza kuhusu miradi ya uwekezaji inayoiingizia mapato Halmashauri pamoja na usimamizi na ukusanyaji wa mapato ambapo mara zote mafunzo hayo yamekuwa yakitolewa na wataalamu kutoka katika idara na vitengo husika.
“Siri kubwa mbili katika kupiga hatua kwenye ukusanyaji wa mapato ni kuwa na mifumo ya uhakika ya ukusanyaji wa mapato Pamoja na kuwajengea uwezo watumishi na kuwasimamia ipasavyo Pamoja na kuhakikisha wanapata stahiki zao kwa mujibu wa sheria Pamoja na kuwapa motisha watumishi wanaofanya vizuri ktika maeneo yao ya kazi ili kupunguza vishawishi wanavyokumbana navyo hasa watumushi katika idara ya Fedha ambayo ndio mhimili mkuu katika Halmashauri zote nchini”. Alisema Kihamia wakati wa mafunzo
Kufuatia heshima hiyo mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero Mhe. David Lugazio Amempongeza Ndg. Kihamia kwa moyo wake na umahiri mkubwa katika kusimamia shughuli za kiutendaji ukilinganisha na wakurugenzi wengine wa Halmashauri zote nchini.
Katika ziara hiyo pia wageni walifanikiwa kutembelea eneo la machinjio ya kisasa linalomilikiwa na Halmashauri ya jiji la Arusha linalojulikana kama Arusha Meat na kujionea namna Halmashauri inavyoweza kujiongezea mapato kupitia mradi huo mkubwa.
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa