Mkuu wa Wilaya ya Wilaya ya Arusha Mhe. Fabian Gabriel Daqarro mwishoni mwa wiki hii amekutana na Maafisa Watendaji wa Kata zote za Jiji la Arusha kuzungumzia kuhusu masuala mbalimbali muhimu yanayotakiwa kupewa kipaumbele katika Wialaya hiii.
Katika Kikao hicho Dc Daqarro ametilia mkazo masuala ya Usalama wa Chakula katika Mitaa yote, Ulinzi na usalama, usimamizi wa miradi ya maendeleo pamoja na utoaji wa taarifa za matukio yasiyo ya kawaida yanayotokea katika kila Kata.
Akizungumza katika kikao hicho alisema “nahitaji kupata takwimu sahihi kutoka katika kila Kata ya mahitaji ya Chakula, kiasi kilichopo na namna ambavyo mmejipanga kukabiliana na upungufu endapo utatokea, kila afisa ugani wa eneo husika ahakikishe anatoa elimu ya kutosha na kufuatilia kuhusu usalama wa chakula katika eneo lake na kuwasilisha taariha hizo katika Ofisi yangu. Sitamuelewa mtendaji ambaye kwa kutokuwajibika kwake kutasababisha njaa ama upungufu wa chakula kwa namna yeyote ile.
Aidha alisisitiza kusimamia miradi ipasavyo ili iwe na ubora na iweze kudumu muda mrefu, kusimamia Usalama wa Kata kwa kutoa taarifa za kila tukio lisilo la kawaida linalotokea kila siku na kudhibiti uingiaji wa wageni kutoka nje ya nchi wanaofika katika Kata.
“Wageni wote wa Nje ya Nchi lazima taarifa zao zifikishwe kwa Afisa uhamiaji wa Wilaya ili kujiridhisha kwamba wameingia nchini kihalali na kuwa na shughuli maalumu iliyowaleta katika maeneo yenu aliongeza”.
Sambamba na hilo alisema si ruhusa kwa Mtendaji wa Kata kutoa mihutasarti kwa ajili ya kumilisha upatikanji wa silaha kwa sababu hivi sasa zoezi hilo limesitishwa mpaka pale Uhakiki wa silaha utakapokamilka hivyo kwa kuwa muombaji ni lazima aanzie kwenye ngazi ya kata si ruksa kwa vikao husika kutoa mihutasari ya aina hiyo.
Mwenyekiti wa Watendaji wa Kata katika Jiji la Arusha Ndg. Suleimani Kikingo alisema kwa umoja watahakikisha kwamba maagizo yote yaliyotolewa wanayatekeleza kwa ufanisi ili kuleta mabadiliko ya haraka na kutoa hudma bora kwa wakazi wa Jiji hili
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa