Na Mwandishi Wetu
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Ndg. Sahili Geraruma amelipongeza Jiji la Arusha kwa kuhakikisha miradi saba ya maendeleo yenye jumla ya Sh. bilioni 3.4 iliyokaguliwa na kuwekewa mawe ya msingi imetekelezwa kwa asilimia 100.
Aidha ametoa pongezi kwa Jiji hilo baada ya kujionea uhalisia wa mradi wa vijana wa kuongeza thamani ya bidhaa za nyuki wa Sessan Enteprices wenye vijana walionufaika na mkopo wa asilimia 10 unaotolewa na halmashauri ya Jiji la Arusha.
Alisema miradi iliyozunduliwa na mwenge huo wa uhuru katika Jiji la Arusha ikiwemo mradi wa maji Terrat-Muriet, Kituo cha Afya Mkonoo, Ukaguzi wa Nyumba ya Waraibu wa dawa za Kulevya sanjari na kuwakabidhi kadi za matibabu za Bima ya Afya 178 kwa warahibu wanaoishi Sobar House nne ni ishara tosha ya kuwa Jiji hilo ni la mfano katika kuhakikisha miradi inatekelezwa kulingana na thamani halisi ya fedha.
Alisema miradi iliyotembelewa na mingine iliyowekwa jiwe la msingi imeonyesha dhahiri kuwa Maendeleo ya wananchi yanakuwa ikiwemo kuimarisha uchumi wa wananchi wa Jiji hilo
"Nawapongeza Jiji la Arusha kwa miradi mliyotekeleza ikiwemo huduma za maji lakini pia kilichotuvutia zaidi ni huu mradi wa vijana wakuongeza thamani bidhaa za nyuki mradi huu ni wa mfano kwasababu fedha za halmashauri za mikopo zimezaa matunda na kuzalisha ajira kwa vijana"
Ukiwa eneo la Murriet mwenge huo uliweka jiwe la msingi mradi wa usambazaji wa maji katika kata hiyo utakaonifaisha wananchi zaidi ya 24,000 ambapo mradi huo upo chini ya Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (AUWSA)
Aidha, mmoja kati ya warahibu eneo la Njiro,Jumanne Ally alitoa rai serikali kuwasaidia warahibu ambao wamepona na wanahitaji kujiajiri au kuajiriwa katika fani mbalimbali nchini kwani baadhi yao ni wasomi na walijiingiza kuvuta unga kutokana na vishawishi vya aina mbalimbali.
"Tunaomba tupewe mikopo katika halmashauri mbalimbali sanjari na kazi kwani hapa kunawasomi na wengine wanaujuzi mbalimbali,tusitengwe bali tupewe nafasi ya kuonyesha kuwa tunaweza kufanya kazi zozote kwaajili ya kujikwamua kiuchumi"
Naye Mkuu wa Wilaya ya Arusha,Said Mtanda alisisitiza wananchi kushirikiana na serikali katika kuinua sekta mbalimbali ikiwemo kujikwamua kiuchumi.
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa