Kuelekea katika zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura, linalofanywa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Halmashauri ya jiji la Arusha kupitia Jimbo la Uchaguzi la Arusha Mjini, wameanza rasmi mchakato wa uboreshaji wa Daftari hilo kwa kutoa Mafunzo kwa Maafisa Waandikishaji wasaidizi ngazi ya Kata.
Akizungumza wakati wa kufungua mafunzo hayo, Afisa Mwandikishaji Jimbo la Arusha Mjini Dkt. Maulid Suleiman Madeni, amewataka Maafisa Waandikishaji hao wa ngazi ya kata kufuatilia kwa umakini mafunzo hayo yanayotolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi ili kuweza kusimamia zoezi hilo kwa umakini na uadilifu ndani ya kata zao.
Dkt. Madeni amesisitiza kuwepo kwa ushirikiano kati ya watendaji wote wa zoezi hilo, serikali, vyama vya siasa na wadau wengine pamoja na kutosita kuomba ufafanuzi au maelekezo katika kazi zao.
Naye Afisa Uchaguzi wa Halmashauri ya jiji la Arusha Bi. Namnyaki Laitetei ameeleza kuwa zoezi hilo linategemea kufanyika kwa muda wa siku 7 tu, kuanzia tarehe 18 -24 Julai, 2019 katika kata 25 za Jimbo la Arusha mjini kukiwa na jumla ya vituo 185 vya kujiandikishia.
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa