Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha Maximilian Iranghe amewataka Madiwani na Wataalam Jiji la Arusha kufanya kazi kwa ushirikiano ili kuwezesha kufanya mambo makubwa ya maendeleo.
Ameyasema hayo alipokuwa akitoa neno la Shukrani kwa Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Songoro Mnyonge na wataalam wa Manispaa hiyo Jijini Dar es Salaam.
Amesema Jukumu kubwa lililobaki kwa Madiwani na wataalam wa Jiji la Arusha ni kujifunza yale mazuri yaliyofanywa na manispaa hiyo na kisha kwenda kuyafanya kwa vitendo.
Meya Maximilian amesema Madiwani hao na wataalam wamefika katika manispaa hiyo kwa lengo la kubadilishana uzoefu wa kuutendaji hasa namna ambavyo miradi ya maendeleo inatakelezwa na ukusanyaji wa mapato unavyosimamiwa.
Kwa upande wake Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Songoro Mnyonge ameshauri kuwa kuna wakati wakufanya siasa na kuna wakati wakufanya maendeleo hivyo vitenganishwe ili malengo na matakwa ya Serikali ya awamu ya Sita yakuwaletea maendeleo wananchi ifanikiwe.
Amesisitiza kuwa katika hatua zakuleta maendeleo ni lazima kuwe na ushirikiano, kuheshimiana na kuaminiana.
Nae, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Arusha Ole Soilel amewashauri Madiwani na Wataalam wa Jiji la Arusha kwenda kufanya maamuzi magumu ili wananchi waendelee kupata maendeleo.
Amesema maendeleo yatapatikana kama siasa haitaingilia shughuli za maendeleo.
Ziara ya Madiwani na wataalam wa Jiji la Arusha Mkoani Dar es Salaam imefanyika kwa lengo la kubadilishana uzoefu wa upangaji Miji, ukusanyaji wa Mapato, shughuli za usafi wa mji, uibuaji wa miradi ya maendeleo ambapo miradi iliyotembelewa ni ujenzi wa standi ya Mwenge, jengo la biashara na kiwanja cha mpira.
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa