Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mjini Mh. Gabriel Daqarro amezungumza na wanafunzi wanaotarajiwa kuhitimu masomo yao ya kidato cha nne mwezi Novemba 2019 katika mahafali ya shule za sekondari za Jiji la Arusha yaliyofanyika mapema leo Tarehe 26 Oktoba 2019 katika viwanja vya Shule ya sekondari Arusha. Mahafali haya yamehusisha shule za sekondari za Serikali na binafsi zilizopo Jijini Arusha.
Serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi wa Mh. Rais Dkt. John Pombe Magufuli ilitoa ahadi ya elimu bila malipo mwaka 2015 na imetekeleza ahadi hiyo hivi sasa wanaotarajiwa kuhitimu elimu ya kidato cha nne novemba mwaka 2019 ni zao la kwanza la elimu bila malipo.
Kwa mwaka 2016 wanafunzi waliohitimu elimu ya kidato cha nne Jijini Arusha walikuwa wanafunzi wapatao 4,447 bali hivi sasa wanaotarajiwa kuhitimu kidato cha nne mwaka 2019 wameongezeka paka kufikia wanafunzi 6,833 ikiwa ni ongezeko kubwa na hii ni kwasababu ya juhudi za Serikali ya awamu ya tano kutoa elimu bila malipo hivyo kupelekea wazazi wengi kupeleka watoto shule.
Akihutubia wanafunzi katika mahafali ya kidato cha nne Mh.Gabriel Daqarro amewaeleza wanafunzi hao kuwa hakuna namna mwanafunzi atajitenga na Mh. Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwani wote ni matunda yake na amewawaomba wanafunzi hao kumrudishia Mh Rais zawadi ya ufaulu wa alama nzuri kwenye mitihani yao ya mwisho ikiwa ni ishara ya kuonyesha juhudi na matokeo chanya ya elimu bila malipo.
Pamoja na kuwahusia wanafunzi Mh. Daqarro amezungumza na walimu wa shule hizo zilizohudhuria mahafali hayo kwa kuwashukuru juu ya juhudi mbalimbali wanazoendelea kuzifanya ili kuleta matokeo chanya katika sekta ya elimu, juhudi hizo zikiwa ni pamija na utaratibu wa namna walivyoanzisha makambi ambayo wamewaweka wanafunzi kwaajili ya kujiandaa na mitihani. Amesema makambi hayo yamekuwa na matokea chanya kwani katika mitihani ya mock wanafunzi hao wamefanya vizuri na kupelekea Jiji la Arusha kuongoza kwa kushika nafasi ya kwanza katika mkoa wa Arusha.
Pamoja na hayo Mh. Daqarro ameeleza kuwa kutokana na changamoto ya upungufu wa chakula mashuleni kuonekana ikikithiri wazazi wahinizwe zaidi juu ya kuchangia chakula cha wanafunzi kwani waraka wa elimu unaelekeza kuwa chakula cha wanafunzi kitagharamiwa na wazazi.
Afisa Elimu Sekondari Jiji la Arusha Ndg. Valentine Makuka ameipongeza serikali ya chama cha mapinduzi chini ya Mh. Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuongeza vyumba vya madarasa kutokea vyumba 448 kwa mwaka 2016 paka kufikia vyumba 500 mwaka 2019. Pia ameishukuru Serikali kwa kuhakikisha adha ya meza na viti imetoweka na sasa kila mwanafunzi ana meza na kiti chake. Pamoja na pongezi hizo ameishukuru serikali juu ya fedha zinazotolewa za elimu bila malipo kwani mwaka 2016 zilikuwa ni 645,573,000 hadi kufikia mwaka 2019 zimeongezeka nakufikia 3,758,192,931.45 Pia ameshukuru ofisi ya mkurugenzi wa Jiji la Arusha kwa kutoa fedha na mbalimbali kama motisha kwa walimu pamoja na kuwapatia mafunzo ya kuwajengea uwezo ambayo kwa sehemu kubwa yameleta matokeo chanya katika sekta ya elimu.
Aidha katika risala ya wanafunzi iliyoandaliwa na kusomwa na mwanafunzi wa kidato cha nne Bi. Mwanaisha Mtwana wanafunzi wamemshukuru Mkuu wa Wilaya Daqarro kwa kuwa mdau mkubwa wa elimu hasa katika kufuatilia kwa ukaribu zaidi maswala ya elimu kuhakikisha kuwa taaluma katika Jiji la Arusha inaimarika na hasa lengo la kuondoa daraja sifuri katika ufaulu linatimia. Wakieleza changamoto zao wameiomba Serikali kuhimiza wazazi wachangie gharama za chakula mashuleni ili kusudi wanafunzi wote wapate utulivu wa akili darasani kwani mototo aliyeshiba anauwezo wa kujifunza na kuelewa vizuri.
Akihitimisha mahafali hayo Dc Daqarro amegawa vyeti kwa wanafunzi waliofanya vizuri katika mitihani ya mock kidato cha nne mwaka 2019 ikiwa ni mwanafunzi mmoja bora kwa kila shule iliyofanya mitihani ya mock lakini pia amegawa vyeti kwa walimu ambao wamefanya vizuri katika masomo yao wanayofundisha hii ikiwa ni mwalimu ambae somo lake limekuwa na ufaulu mzuri kwenye mitihani ya Mock.
Pichani: Mh. Daqarro watatu kulia mstari wa mbele akiwa na wanafunzi wakiume waliotunukiwa vyeti vya ufaulu mzuri katika mitihani ya Mock kidato cha nne 2019
Pichani: Mh. Daqarro watatu kulia mstari wa mbele akiwa na wanafunzi wakike waliotunukiwa vyeti vya ufaulu mzuri katika mitihani ya Mock kidato cha nne 2019
Pichani: Mh. Daqarro watatu kulia mstari wa mbele akiwa na walimu ambao wamefanya vizuri katika masomo yao wanayofundisha hii ikiwa ni mwalimu ambae somo lake limekuwa na ufaulu mzuri kwenye mitihani ya Mock 2019.
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa