Pichani: Kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa Ndg. Mzee Kongea Ali (Kushuto) akikabidhi chandarua kwa mkazi wa kata ya Moivaro wakati wa uzinduzi wa mradi wa wodi ya wazazi kituo cha afya moivaro wenye thamani ya shilingi milioni 106
Pichani: Mkurugenzi wa Mamlaka ya maji safi na maji taka mkoa wa Arusha (AUWSA) Mhandisi Ruth Koya akionyesha maendeleo ya mradi wa ujenzi wa tanki kubwa la maji lililopo mlima Burka kwa kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa Ndg.Mzee Kongea Ali
Pichani: Kiongozi wa mbio za mwenge Kitaifa Ndg.Mzee Kongea Ali akiweka jiwe la msingi kwenye mradi wa ujenzi wa ofisi ya kata ya Kati wenye thamani ya shilingi milioni 224.
Pichani: Meneja wa wakala wa barabara za mijini na vijijini Tanzania (TARURA) mkoa wa Arusha Mhandisi Fodia Mwankenja akikabidhi nyaraka za mradi wa ujenzi wa daraja la Oljoro Murriet wenye thamani ya shilingi milioni 227 kwa kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa wakati wa uzinduzi wa mradi huo.
Pichani: Kiongozi wa mbio za mwenge Kitaifa Ndg. Mzee Kongea Ali akitoa ujumbe wa Mwenge punde baada ya kuweka jiwe la msingi katika ujenzi wa jengo la utawala katika shule ya sekondari Naura iliyopo kata ya Lemara.
***********************************************
Katika Jiji la Arusha Mwenge wa Uhuru umekimbizwa katika kata kumi (10) kati ya ishirini na tano (25) ambapo ni sawa na urefu wa kilometa 93.9.
Mwenge wa Uhuru umepita katika miradi nane (8), kati ya miradi hiyo miwili (2) imezinduliwa, miradi miwili (2) imewekewa jiwe la msingi na miradi minne (4) imetembelewa.
Miradi yote nane (8) ina thamani ya shilingi Bilioni 521.28
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa