Na Mwandishi Wetu
Mbunge wa Viti Maalumu Jimbo la Arusha Kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Mh. Zaituni Swai ametoa msaada wa vitu vyenye thamani ya Sh. Milioni 2 yakiwemo Mashuka ya hospitali, vitakasa mikono, ndoo za kunawia mikono,sabuni na vifaa vinginevyo katika kituo cha afya Ngarenaro ikiwa ni kuunga mkono jitihada za Halmashuri ya Jiji la Arusha na Serikali kwa ujumla katika kuboresha sekta ya Afya Jijini Arusha.
Akikabidhi msaada huo Mh. Swai alisema kuwa anaunga mkono Jitihada za Serikali ya awamu ya Sita za kukuza na kuboresha sekta ya afya na kuwezesha wagonjwa kupata huduma bora wafikapo hospitalini hapo.
Alisema kuwa amefurahishwa na huduma bora zinazotolewa katika hospitali hiyo na huku akiwatia moyo na kuwapongeza wauguzi wa hospitali hiyo kwa kazi kubwa na nzuri wanayofanya.
Mganga Mfawidhi hospitali ya Ngarenaro Dkt. Jackson Katunzi akipokea msaada huo kwa niaba ya Mganga Mkuu Jiji la Arusha Dkt. Kheri Kagya alisema kuwa wamefurahi kwa msaada huo na kwamba vifaa hivyo vitasaidia kuongeza chachu ya upatikanaji wa huduma bora hospitalini hapo.
Aliongeza kuwa msaada wa vifaa vya kujikinga na Ugonjwa wa Virusi vya Korona (UVIKO19) umefika wakati sahihi kwani itasaidia kupunguza maambukizi ya wimbi la tatu la ugonjwa huo hatari, huku akiwataka wananchi kuchukua hatua zote stahiki kujikinga na ugonjwa huo.
PICHANI: Mganga Mfawidhi hospitali Ngarenaro Ndg. Jackson Katunzi akipokea msaada wa mashuka ya hospitali, vitakasa mikono n.k kutoka kwa Mbunge Mhe. Zaituni Swai
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa