Na Mwandishi Wetu
WADAU wa Maendeleo katika Jiji la Arusha wameungana na Meya wa Jiji la Arusha , Madiwani pamoja na Wataalam wa Halmashauri ya Jiji la Arusha katika uzinduzi wa Kampeni ya Usafi wa mazingira katika soko la Kilombero.
Kampeni hiyo ni mwanzo wa muendelezo wa kufanya usafi katika Kata 25 za Halmashauri ya Jiji la Arusha
Meya wa Jiji la Arusha Maximilian Iranqhe alisema kuwa lengo kampeni hiyo ni kuhamasisha usafi katika Jiji la Arusha na hatimaye kufanya Jiji la Arusha kuwa mfano kwa mazingira safi ya Utalii na kuvutia watalii wa ndani na nje ya nchi.
Mhe. Maxmillian Iranqhe anasema ili kuandaa mazingira mazuri ya Utalii ni muhimu kila mmoja kujali usafi Kwa kufanya usafi katika Makazi wanayoishi na mahala pa kazi.
Mhe. Iranqhe amewataka Wataalam wa Afya na Maafisa Afya kutoka ofisini nakwenda kusimamia usafi katika Kata za Halmashauri ya Jiji la Arusha.
Amemtaka Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji kusimamia na kufuatilia utekelezaji wa agizo hilo kwamba usafi Jiji la Arusha unawezekana.
Mhe. Iranqhe ameongeza kwa kusema kuwa usafi ni kichocheo cha maendeleo na fursa mbalimbali za kiuchumi kwa Wananchi pamoja na kivutio cha Utalii.
Katika hatua Nyingine Mh .Meya alikabidhi vifaa vya usafi kwa Madiwani wa Kata 25 za Jiji la Arusha ikiwa ni kuwezesha kuhamasisha wananchi wa Kata zao kufanya usafi katika Kata zao.
Denis Mwita ni Katibu wa Chama cha mapinduzi Wilaya ya Arusha anasema kuwa hatua hiyo inaonyesha kuwa Viongozi na madiwani waliochaguliwa kupitia CCM wanania njema ya kuleta maendeleo katika Jiji la Arusha.
Kampeni hiyo iliungwa mkono na wadau wa Taasisi mbalimbali wakiwemo NMB , TANAPA,CRDB , AICC, AZANIA BANK, ambapo baadhi ya Taasisi zilichangia vifaa vya usafi ikiwa ni matenki ya uchafu na mafagio ya Usafi.
PICHANI : Wadau, Wananchi, Viongozi, na wataalam Jiji la Arusha Waliposhiriki zoezi la uzinduzi wa kampeni ya usafi katika Kata zote 25.
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa