Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Jiji la Arusha Dkt. Simon Chacha leo Tarehe 22 Novemba, 2018 amefungia utoaji wa huduma katika clinic inayofahamika kwa jina la ARUSHA IVF AND FERTILITY CLINIC inayoshughulika na huduma ya upandikizaji wa mimba kwa kina mama kilichopo maeneo ya Uzunguni kata ya Sekei Jijini Arusha.
Dkt. Chacha amechukua hatua hiyo mara baada ya mmiliki wa kituo hicho Dkt.Sally Kukaidi amri ya kutoa mabango yake ya matangazo na kuendelea kutoa huduma kinyume na sheria kwani bado hajakamilisha taratibu za usajili wa kituo hicho kutoka Wizara ya Afya kabla ya huduma kuanza kutolewa ambapo kimekuwa kikitoa huduma kwa takriban miaka miwili sasa.
...............................................................................................................................
“Tumeamua kutoa haya mabango kwani mmiliki wa kituo hiki amekuwa akikaidi amri ya kuyatoa kama ambavyo mara kwa mara tumekuwa tukimwelekeza na kumtaka kufanya hivyo na amekuwa akisambaza mawasiliano ya kituo chicho kwa kutumia mabango haya pamoja gari aina ya NOAH lenye namba za usajili T989 CGA ambalo tumeshatoa taarifa kwa vyombo vya usalama barabarani endapo likionekana likamatwe mara moja ” alisema Mganga Mkuu huyo.
..........................................................................................................
Aidha Dkt. Chacha ameongeza kwa kusema kuwa mmiliki wa kituo hicho anaishi Nchini Uganda na anafanyia kazi zake Dar es salaam hivyo amekuwa akiacha mtu katika clinic hiyo ambaye amekuwa akiwasiliana na wateja moja kwa moja kisha ndio afunge safari kuja kutoa huduma Jijini Arusha na kwa sasa hatua za usajili wa kituo hicho zimesitishwa mpaka pale itakapoamuliwa vinginevyo.
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa