Mganga Mkuu wa Jiji la Arusha Dkt. Simon Chacha amefungia utoaji wa huduma ya afya katika zahanati inayofahamika kwa jina la Faraja Dispensary iliyopo kata ya Levelosi baada ya kubaini mapungufu mbalimbali wakati wa ziara yake ya kushtukiza aliyoifanya leo Tarehe 25/07/2019 akiambatana na kamati ya Afya ya Jiji la Arusha.
Akikagua hali ya utoaji wa huduma katika zahanati hiyo inayomilikiwa na Dkt. Sabina Mtweve, Mganga Mkuu wa Jiji alibaini mapungufu mbali mbali ikiwemo zahanati hiyo kutokuwa na watumishi wenye sifa, kutosajiliwa kwa kliniki ya meno na uchafu uliokithiri katika zahanati hiyo pamoja na msimamizi wa kituo hicho kutotuma taarifa katika mfumo wa kitaifa wa kutolea taarifa za magonjwa (EIDSR) kama maelekezo ya Wizara ya Afya inavyoelekeza.
Kufuatia mapungufu hayo Dkt. Chacha alilazimika kusitisha utoaji wa huduma katika Zahanati hiyo.
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa