Mkuu wa Wilaya ya Arusha Felician Mtahengerwa amewagiza Wakala wa Barabara za Vijijini na Mjini(TARURA)Wilaya ya Arusha kutengeneza daraja la Mtaa wa Suye kata ya Olorien iliyoaribiwa na mvua zinazoendelea kunyesha.
Maaguzi hayo ameyatoa alipokuwa akikagua maeneo mbalimbali yaliyoathirika na mvua katika Jiji la Arusha.
Lengo la ukaguzi huo ulikuwa nikuona kwa namna gani miundombinu hasa ya barabara na makazi ya watu yalivyoathirika na mvua ili Serikali iweze kuchukua hatua za haraka pale inapolazimu kufanya hivyo.
Aidha, Mkuu wa Wilaya ameendelea kutoa rai kwa wananchi kuendelea kuchukua taadhari za mvua hizo zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali.
Kwa upande wake,Kaimu Mkurugenzi Jiji la Arusha Shabani Manyama amesema tayari halmashauri imeshatoa milioni 17 kwa ajili ya ukarabati wa eneo hilo.
Amesema fedha hizo zipo hatua za mwisho za ukamilishwaji na ukikamilika Halmashauri watawakabidhi TARURA kwa utekelezaji zaidi.
Halmashauri ya Jiji la Arusha imeshatenga kiasi cha Milioni 380 kwa ajili ya kukabiliana na athari zinazotokana na mvua zinazoendelea kunyesha.
Ziara ya ukaguzi huo imefanyika katika maeneo mbalimbali ikiwemo daraja la mtaa wa Suye, Njiro kwa Msola, mtaa wa mbondeni na Kituo cha afya Murriet.
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa