Waziri wa Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt.Damas Ndumbaro amesema uwanja wa mpira wa miguu (AFCON) ni wa wananchi ndio maana Serikali inawashirikisha kwa kila hatua.
Hayo amesema, alipokuwa akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mirongoine Kata ya Olmot, Jijini Arusha.
Uwanja huo ni maono na fikra za Rais Samia Suluhu Hassani katika kuhakikisha sekta ya michezo inakuwa na kushamiri.
Amesema AFCON iliamzishwa 1977 na ni mara ya kwanza kufanyika katika ukanda wa Afrika Mashariki kwa nchi za Tanzania, Uganda na Kenya.
Katika eneo hilo kutakuwa na miundombinu mbalimbali ya Hoteli, kumbi za starehe, maduka makubwa.
Uwanja huu utaenda kukuza zaidi sekta ya utali kwani uwanja utakuwa kivutio kwa watu wengi.
Amesisitiza zaidi kuwa, uwanja huo utakuwa ni uwanja wa michezo kwani kutakuwa na sehemu za michezo mbalimbali kama vile riadha, mpira na pete.
Amemtaka Mkandarasi na mshauri mwelekezi kujenga uwanja wenye ubora na utakao kamilika kwa wakati.
Pia, amemtaka Mkandarasi kuhakikisha ajira zote wanapewa vijana wa Arusha hususani wa Kata ya Olmoti.
Uwanja huu, utabeba taswira ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, hivyo ni uwanja ambao sio wa kawaida.
Aidha, amesema kwa yale maeneo ya wananchi ambayo yatachukuliwa kwa ajili ya uwekezaji wa uwanja huo watalipwa stahiki zao halali.
Nae, Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni,Sanaa na Michezo Gerson Msigwa amesema uwanja huo utagharimu kiasi cha Bilioni 286 hadi kukamilika kwake na utajegwa kwa miaka 2.
Amesema katika eneo hilo kuna viwanja 14 vilivyotegwa kwa ajili ya ujenzi wa Hotel hivyo amewakaribisha wawekezaji kuwekeza katika maeneo hayo.
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Arusha Felician Mtahengerwa akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha Paul Makonda amesema uwanja huo utaleta fursa nyingi kwa Mkoa na hivyo kupanua wigo wa biashara.
Pia, sura ya Mkoa wa Arusha itabadilika na uwanja huo utakuwa kivituo kwa wageni wengi.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Arusha Wilfred Soileli amewataka wananchi wa Kata ya Olmot kuwa walinzi wa vifaa vitakavyotumika katika ujenzi wa uwanja huo.
Hafla ya kumkabidhi Mkandarasi eneo la ujenzi wa uwanja wa michezo Arusha umefanyika baada ya Mkandarasi kusaini mkataba wa ujenzi na Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo mnamo Machi 16,2024 Jijini Dar es Salaam.
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa